MSANII wa vichekesho kutoka Kundi la Vituko Show,
Ismail Makombe ‘Mapembe’, anadai kuingizwa mjini na staa mwenzake, Mussa
Yusuf Kitale ‘Mkude Simba’ kwa kumuahidi kumchangishia pesa na mwisho
kuingia mitini.
“Ndugu yangu kweli hujafa hujaumbika, naumwa kweli nakosa msaada wa karibu kutoka kwa wasanii wenzangu na leo naishia kutoa lawama huku wengine wakiniingiza mjini kama alivyonifanyia Kitale aliyeniahidi kunichangishia pesa na kunikataza kuombaomba kwa madai ya kuitia aibu tasnia yetu lakini mpaka leo.”
Staa wa Maigizo upande wa vichekesho, Mussa Yusuf Kitale ‘Mkude Simba’ akiwa kwenye ofisi za Global publishers.
Baada ya kupata madai hayo, paparazi wetu alimtafuta Mkude Simba
‘Kitale’ na alipopatikana alisema: “Ni kweli Mapembe nilimuahidi
kumchangishia pesa ila baada ya wazo hilo kulifikisha kwenye chama chetu
cha komedi viongozi waligoma kumsaidia kwa madai kuwa yeye siyo
mwanachama wao na hata kipindi chama kinaanzishwa aligoma kujiunga kwa
kuona hakina maana hivyo nao wamekataa, kwa hiyo hana sababu ya
kunilalamikia.”
Post a Comment