Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BATULI NA MTUNIS PENZINI TENA


WASANII wawili wa filamu, Nice Mohamed ‘Mtunisi’ na Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ ambao walikuwa wapenzi kabla ya kuachana na mwanaume huyo kuoa, sasa wamerudiana rasmi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilicho jirani na wasanii hao kimesema wawili hao hivi sasa wanapika na kupakua.Kilisema baada ya kurudiana, kwa sasa wanaishi pamoja kama mume na mke maeneo ya Sinza, jijini Dar es Salaam huku wakiishi kwa amani na upendo.

 Yaani sasa hivi Batuli na Mtunisi wana mahaba niue kwani wanaishi pamoja wanaamka na kulala wote maeneo ya Sinza-Mawela lakini wanafanya kuwa ni siri yao, hawataki watu wajue
kilisema chanzo hicho.
Hivi karibuni Batuli aliweka picha ya Mtunisi katika akaunti yake kwenye mtandao wa Instagram na kuandika maneno haya
 Alichokipanga Mungu hakuna wa kukipangua.
Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, Batuli alisema hawezi kuzungumzia katika vyombo vya habari kwa vile mambo hayo ni maisha yake binafsi.
Kwa upande wake, Mtunisi alicheka na kudai kusikia kutoka kwa watu juu ya mwenzake kuweka picha yake mtandaoni na kuandika maneno ya kimahaba, kitu alichosema hawezi kuzuia nafsi ya mtu kumuweka moyoni.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top