Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LUIS SUAREZ AANZA KUJITETEA JUU YA TUHUMA ZA KUMNG'ATA MCHEZAJI MWENZIYE UWANJANI

 


Wakati kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka duniani FIFA ikimtaka mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay Luis Suarez, pamoja na shirikisho la soka la nchi hiyo kuwasilisha ushahidi wa kupinga shutuma za kumng’ata beki wa timu ya taifa ya Italia ya Gorgio Chiellini, kabla ya saa kumi na moja kwa saa za nchini Brazil, mshambuliaji huyo ameanza kujitetea kupitia vyombo vya habari.
Luis Suarez, ambaye amechukuwa nafasi kubwa katika vyombo vya habari hii leo kufuatia tukio la kumng’ata mchezaji wa Italia wakati akiwa kwenye majukumu ya kulitetea taifa lake hapo jana, amesema anashangazwa na taarifa zinazoendelea kuandikwa na kuzungumzwa kwenye vyombo vya habari.
Suarez, amesema hakumng’ata Chiellini kama mashabiki wanavyopokea taarifa hizo, bali waligongana kwa bahati mbaya na beki huyo wa klabu bingwa nchini Italia Juventus, hivyo kinachoendelea dhidi yake kwa sasa anakichukua kama uonevu wa kutaka apewe adhabu kali kutoka FIFA.
 “Nakumbuka tukio lilivyokuwa, wakati mpira uliopigwa kutoka sehemu ya kulia kwangu ukiwa angani nilikuwa nautazama, hivyo sikuangalia pembeni na sikujua nani anakuja kunikabili, lakini nilipogeuka nilikutana na Chiellini na kwa bahati mbaya niligongana nae katika sehemu za bega lake la upande wa kushoto. Amesema Suarez.
Wakati FIFA kupitia kamati ya nidhamu ikisubiri ushahidi wa Luis Suarez kwa njia ya maandishi, imeanza kuhisiwa huenda mshambuliaji huyo wa klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza akaadhibiwa kwa kufungiwa kucheza michezo kadhaa ambayo itakuwa chini ya shirikisho hilo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top