Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAMBO YAZIDI KUMUWIA MAGUMU KAJALA, SASA ATAMANI KUIKIMBIA BONGO.



Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja amefunguka kuwa yuko Bongo kwa kuwa ndipo nyumbani kwao lakini hana hamu ya kuendelea kuishi nchini kutokana na kuzushiwa mambo kila kukicha.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko wikiendi iliyopita, mwigizaji huyo alisema anapenda awe na maisha ya furaha na wanawake wenziye kwa kubadilishana mawazo ya hapa na pale lakini kwa sasa hana upendo huo kwa kuwa kuna watu wanaishi kwa kutegemea bifu.
 
“Unajua inauma sana, unaenda klabu unamkuta mtu ambaye huko nyuma alikuwa shoga’ko, kula, kuvaa na kila aina ya ushirikiano mnapeana, sasa mnakuja kugombana, kiukweli roho huwa inauma ndiyo maana nashindwa hata kwenda klabu kuepusha mengi, nasubiria viza yangu itoke nisepe zangu China,” alisema Kajala.
Kwa muda mrefu kumekuwa na ugomvi usiokwisha kati ya Kajala na mwigizaji mwenzake, Wema  Sepetu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top