Miinza Matoki aolewa kuwa mke wa tisa.
Mke
wa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Miinza Matoki (20), ameikimbia
ndoa yake kisa kikielezwa kuwa ni mauzauza ya kichawi anayokutana
nayo.Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Minza ambaye ni mkazi wa Manyoni
mkoani Singida alisema wazazi wake walimuozesha kwa ‘kibabu’ aliyemtaja
kwa jina moja la Samson ambaye aliwahi kuoa wanawake nane kabla yake
hivyo yeye kuwa wa tisa.
Alisema
siku chache baada ya kuolewa alianza kuona mauzauza usiku ambapo alidai
alikuwa akichezewa mwilini na watu ambao hakuwafahamu wenye sura za
kutisha huku wakiwa wamevaa nguo nyeupe.
Mwanamke
huyo alisema mchana alipokuwa akienda kuchunga ng’ombe akirudi nyumbani
alikuta kinyesi cha binadamu kwenye begi la nguo zake.“Siku moja
niliamshwa usiku saa kumi na kuambiwa niende kisimani kuchota maji,
nikakutana na mtu aliyevaa nguo nyeupe, nikamsalimia hakuitika,
nikachota maji na kuondoka, nilipotazama nyuma sikumuoana nikaanguka na
kupoteza fahamu.“Nilijikuta
nikiwa sehemu ambayo sikuifahamu, palikuwa na watu wengi waliovaa nguo
nyeusi ambapo nilishikwa mkono na mtu ambaye nilikuwa namfahamu kwamba
ni mtoto wa mjomba wangu, akanipandisha kwenye fisi huku nikiwa
nimevalishwa nguo nyeusi na kufungwa hirizi mwilini, nikaamriwa nikamuue
mama yangu na baada ya kupanda fisi tulienda kwa mama yangu, mtu
niliyeongozana naye alikuwa na utaalamu wa kutosha.
“Zoezi la kumuua mama lilishindikana ndipo nikaganda kwenye mlango na yule niliyeenda nayeyeye aliondoka na kuniacha.
“Mama
alipoamka asubuhi alinikuta mlangoni nikiwa sijielewi huku nimevaa nguo
nyeusi ‘kaniki’ na kufungwa hirizi, alimwita mganga akanitoa pale na
kuninywesha dawa lakini sikupona ndipo nikapelekwa kwa mchungaji
kuombewa.
“Baada
ya hapo nilirudi kwa mume wangu na kuchukua nguo zangu na kutoroka
ambapo niliomba lifti kwenye gari la mkaa na kushushwa Ubungo jijini
Dar,” alisimulia mwanamke huyo huku akiapa kutorudi kwa mzee huyo ambaye
hakupatikana kwani hana simu.
Kwa
sasa mwanamke huyo amehifadhiwa kwa Mwenyekiti Mtaa wa Shimo la Udongo,
Kurasini kwa mama Felister Komba ambaye baada ya kufika kwake
alimpeleka Kituo cha Polisi cha Kurasini na kufunguliwa faili la taarifa
lenye namba KUR/340/2014.
Post a Comment