Kaka wa marehemu (Munili Omary), Omary akiwa kwenye msiba wa mdogo wake.
Tukio hilo lililoacha simanzi kwa wanafamilia na wakazi wa Kitongoji cha Mpakani lilitokea saa 2 asubuhi ya Juni 18, mwaka huu.
WAKATI wanaharakati wanaendelea kupiga kelele kuhusu kushamiri kwa vitendo vya unyanyasaji kwa watoto duniani kote, mwanamke aliyetajwa kwa jina la Amina Hamis, mkazi wa Kata ya Kwembe, Malamba Mawili Kitongoji cha Mpakani, Kinondoni jijini Dar ametiwa mbaroni kwa madai ya kumuua kwa kipigo mtoto Munili Omar (6).
Awali,
habari za madai ya mtoto huyo kuuawa yalitua kwenye chumba cha habari
cha Uwazi ambapo mwandishi wetu alifunga safari hadi eneo la tukio.
Mtu wa kwanza kuonana naye alikuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, James Nyanda ambaye alikiri kutokea kwa mauaji hayo ya kikatili.
Mtu wa kwanza kuonana naye alikuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, James Nyanda ambaye alikiri kutokea kwa mauaji hayo ya kikatili.
Mwanamke
aliyetajwa kwa jina la Amina Hamis, mkazi wa Kata ya Kwembe, Malamba
Mawili Kitongoji cha Mpakani, Kinondoni jijini Dar anayeshikiliwa kwa
kesi ya kumuua mwanaye.
MAMA ADAIWA KUYUMBISHA MAELEZO
Akizungumza na gazeti hili kuhusu mkasa mzima wa mtoto huyo, mwenyekiti huyo alisema:
“Ilikuwa
saa 2 asubuhi ya Juni 19, nikiwa nyumbani kwangu nilipigiwa simu na
msamaria mwema na kunifahamisha kwamba nyumbani kwa Juma Omar kulikuwa
na msiba wa kutatanisha uliotokea jana yake, yaani Juni 18 asubuhi.
“Baada
ya kupata taarifa hiyo, saa 3 asubuhi nilikwenda eneo la tukio na
kukutana na Amina anayetuhumiwa kufanya mauaji hayo akiwa na baadhi ya
ndugu, majirani na wifi yake anaitwa Faudhia Idd. Nilihoji kuhusiana na
kifo hicho, wakaniambia mtoto alifariki dunia baada ya kuanguka.
“Niliuliza
sababu ya kukaa na maiti hiyo ndani kwa siku nzima bila kuipeleka
hospitali, nikajibiwa alikuwa akimsubiri mumewe ambaye hakuwepo.
“Niliomba
namba za simu za mumewe ili nimjulishe msiba huo, akanipa. Nilimpigia,
nikamweleza mwanaye amefariki dunia hivyo arejee nyumbani, akaniambia
alikuwa safarini Ilula (Iringa) hivyo mtoto azikwe tu.
“Alipotoa
kauli ile nilishangaa sana, nikamwambia arudi nyumbani kwa sababu
tusingeweza kumzika mwanaye bila yeye kuwepo, akasema atarudi.”
POLISI WAPIGIWA SIMU KUJULISHWA
Mwenyekiti
huyo aliendelea kusema: “Kutokana na utata wa kifo hicho niliamua
kuwapigia simu polisi wa Kituo cha Mbezi Kwayusuf ambao walifika,
wakamchukua Amina, wifi yake na mwili wa mtoto huyo wakaupelea
kuuhifadhi Hospitali ya Tumbi (Kibaha) kisha mama huyo kushikiliwa
kituoni kumsubiri mumewe.
“Mume
ambaye hakujua kiini cha kifo cha mwanaye alipowasili aliunganishwa na
mkewe kituoni lakini polisi walishindwa kuwa na ushahidi wa mtoto huyo
kuuawa hivyo waliandika RB ya KIFO CHA UTATA kisha wakaruhusiwa kurudi
nyumbani kuandaa taratibu za mazishi ya mtoto wao,” alisema mwenyekiti.
AKINA MAMA WA KITONGOJI WAKATAA
Mwenyekiti
huyo aliendelea kusimulia kwamba, kufuatia akina mama wa Kitongoji cha
Mpakani kutilia shaka kifo cha mtoto huyo waliyedai alikuwa akinyanyaswa
na kupigwa mara kwa mara, kurushwa kichura, kufungiwa ndani, kunyimwa
chakula, kukataa kumpeleka hospitali kwa madai angelazwa jambo ambalo
hakuhitaji kulisikia, waliamua kumbana wifi yake Faudhia, ndipo akaweka
wazi kwamba kifo chake kilitokana na kipigo!!!
Kwa
mujibu wa maelezo ya Faudhia, siku ya tukio, marehemu Munili ambaye
mama yake mzazi anaishi Nzega, Tabora, alikojoa kitandani ndipo
mtuhumiwa akampeleka sebuleni na kuanza kumchapa mwilini na kichwani
hadi akakata roho mbele yake.
FAUDHIA ALIFUNGUKIA UWAZI
Akizungumza na Uwazi msibani hapo, Faudhia alisema:
“Siku
ya tukio ambayo ilikuwa Juni 18, Munila alikojoa kitandani ndipo wifi
alimtoa sebuleni na kuanza kumchapa kwa kutumia mkanda. Alipoona mtoto
ametulia, aliniita na kuniambia Munili alianguka hivyo niende nikamwite
nesi anayemiliki duka la dawa mtaani, nilimwona Munili akitokwa povu
mdomoni, jeraha la kupigwa na mkanda kwenye paji la uso na shingoni,
nilipomuuliza alipatwa na nini akaniambia alianguka.
“Nilipofika
kwa nesi akaniambia kama mtoto alizidiwa tumpeleke hospitali, nilirudi
nyumbani na kumweleza wifi, ndipo akachukua maji ya baridi na kummwagia
Munili lakini hakuamka, alichukua kitenge akampepea lakini Munili
alitulia kimya.
“Wifi
akanituma niende kumwita mama Aneth ambaye ni jirani, alipofika
alimwangalia mtoto akashauri akaitwe mjumbe ambaye hakuwepo. Nikamfuata
Shehe Mpitanga ambaye alipofika na kumwangalia mtoto akasema
alishafariki dunia, wifi akaanza kulia.”
Faudhia
aliongeza kuwa, alipowaeleza ukweli akina mama kuhusiana na tukio hilo,
wifi yake alitoka ndani na kutaka kutoroka lakini walifanikiwa kumnasa
ndipo nilichukuliwa mimi, kaka (baba wa marehemu), tukapelekwa tena
polisi ambako nilieleza kilichotokea, wakaamua kuwashikilia wao hadi leo
(Juni 21, mwaka huu).
KAMANDA WA POLISI AZUNGUMZA
Kamanda
wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura alipopigiwa simu na
kuulizwa kama alikuwa na taarifa ya mauaji hayo alisema hakuwa na
taarifa ila atafuatilia.
Post a Comment