Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akizungumza jambo na Mwenyekiti mpya wa bodi ya
Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Prof. Lucian Msambichaka (wa pili
kushoto) wakati alipozindua bodi mpya ya kituo hicho Jumatatu wiki hii
jijini Dar es Salaam. Wengine ni Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu
(kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bi. Juliet kairuki (katikati) na
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw. Raymond Mushi (kushoto).
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya
wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Jumatatu wiki hii
jijini Dar es Salaam. kushoto ni Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Prof.
Lucian Msambichaka; Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu
(nguo nyekundu), Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw. Raymond Mushi (kulia
katikati) na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Florens Turuka
(kulia).
Mwenyekiti
mpya wa bodi ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Prof. Lucian
Msambichaka (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa
kituo hicho, Bi. Juliet Kairuki (kushoto) pamoja na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu
(katikati) wakati wa uzinduzi rasmi wa bodi mpya ya kituo hicho Jumatatu
wiki hii jijini Dar es Salaam uliofanywa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
chanzo:jiachie
Post a Comment