Grace Loy (20), mkazi wa Mwananyamala Mchangani, aliyepigwa risasi katika paja la kulia wakati wa vurugu iliyotokea.
MAMA mzazi wa binti aliyesababisha
wasichana wawili kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na polisi baada ya
kushiriki ngoma maarufu ya Kanga Moko iliyopigwa marufuku, huko
Mwananyamala Kisiwani jijini Dar es Salaam, amefunguka na kusema kuwa
hakukuwa na sherehe yoyote nyumbani kwake siku hiyo ya tukio.
Mama huyo, Rehema Aziz alisema waliojeruhiwa walikuwa wakisherehekea kuolewa
kwa mwanaye aitwaye Aziza Aziz, ambao walikuwa ni marafiki zake na
walifanya hivyo kwa mujibu wa mila za watu wa Pwani, za kucheza na
kufurahi wakizunguka mitaani, lakini bila kufanya fujo yoyote. “Huo
ulikuwa ni Mdundiko wa kawaida, tokea zamani tulikuwa hatuombi kibali na
wao walifanya hivyo kama mila zinavyosema, siku ya tukio Juni 18, mwaka
huu hatukuwa na sherehe hapa nyumbani isipokuwa jana yake ndiyo
kulikuwa na sherehe ya kumpa zawadi mwanangu.
Majeruhi
mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Zawia Hamis (20), mkazi
Mwananyamala anayedai kupigwa risasi tumboni na kwenye makalio.
“Tukio la Juni 18, wasichana ambao ni
marafiki zake mwanangu ambaye kwa sasa yupo kwa mume wake, walikuwa
wakisherehekea wenyewe kivyao, bila mimi kujua, lakini hata hivyo mbona
ilikuwa ni mapema mno, saa kumi jioni na walikuwa ni wanawake tu,”
alisema mama huyo.
Kwa upande wake majeruhi Grace Loy
(20), mkazi wa Mwananyamala Mchangani, alisema anachokijua ni kwa
alipigwa risasi katika paja la kulia wakati huo wa vurugu ya kuwataka
watawanyike.
“Sisi tulikuwa tukiwasindikiza watu
wa tarumbeta ambao walikuwa wanaume, tuliobaki tulikuwa wanawake na
hakukuwa na vurugu wala hatukumpiga askari ila sisi tumepigwa risasi
kama swala,” alisema Grace.
Majeruhi mwingine aliyejitambulisha
kwa jina la Zawia Hamis (20), mkazi Mwananyamala anayedai kupigwa risasi
tumboni na kwenye makalio, alisema ameshangazwa na kitendo hicho.
Walisema ni jambo la ajabu kuwa polisi walitumia nguvu kubwa dhidi ya wanawake waliokuwa hawana silaha yoyote.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho,
Husna Nondo alisema watu hao hawakuwa na kibali cha aina yoyote na
kusisitiza kuwa serikali imeshapiga marufuku ngoma za Kanga Moko hivyo
amewataka wananchi kufuata agizo hilo la serikali.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi
Kinondoni, Camilius Wambura alipoulizwa juu ya suala hilo, alisema
upelelezi unaendelea ili kubaini tatizo
Post a Comment