Colombia
ilikamilisha mechi zake za makundi kwa kishindo ilipoicharaza japan
mabao manne kwa moja na kusalia kileleni mwa kundi C na alama zote 9
Timu
hiyo ambayo ilikuwa imekwisha fuzu kwa kushiriki katika mechi za timu 16
bora haikulegeza kamba kufuatia mori ya Japan kusajili ushindi dhidi
yao..
Japan
ilihitaji ushindi ili kuweza kwendelea kushiriki kombe hili la dunia
lakini Juan Cuadrado aliifungia Colombia kupitia mkwaju wa penalty baada
ya Adrian Ramos kuchezewa visivyo na Yasuyuki Konno mbele ya lango na
akaiweka Colombia kifua mbele .
Muda
mfupi tu kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza, mshambulizi wa
Mainz Shinji Okazaki alifufua matumaini ya Japan kwa kufunga bao kwa
kichwa.
Bao
hili liliwatamausha Colombia ambao sasa walikaza buti na kufunga mabao
matatu bila ya jibu ungedhani wanatafuta tiketi ya kufuzu kwa mkondo
ujao.
Jackson Matinez alirejesha uongozi wa Colombia kabla ya kuongeza bao la tatu kwa Colombia dakika ya 82.
James
Rodriguez alihakikisha Colombia imejizolea alama zote tatu katika mechi
za makundi na kuwa taifa la pili kufanya hivyo baada ya Uholanzi, kwa
kufunga bao la nne mnamo dakika ya 89.
Colombia
itachuana na mshindi wa pili wa kundi D ambaye ni Uruguay baada ya timu
hiyo ya Luiz Suarez kuifungisha virago mabingwa mara nne wa kombe la
dunia Italia ilipoilaza 1-0.
Ugiriki ilifuzu kama mshindi wa pili katika kundi C na hivyo sasa itakwaruzana na washindi wa kundi D Costa Rica .
Kutokana na kichapo hicho Italia iliungana na Uingereza kama timu zilizobanduliwa nje baada ya mkondo wa kwanza .
Aidha Afrika kufikia sasa haina mwakilishi katika mkondo wa pili wa kombe la dunia .Chanzo BBC Swahili
Post a Comment