SMALL BOYS, MSHIKAMANO, PACHOTO ZAPIGWA FAINI RCL
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zimezipiga faini ya kati ya sh. 300,000 na sh. 500,000 klabu za Mshikamano FC, Pachoto Shooting Stars, Town Small Boys na Kiluvya United kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo viongozi, wachezaji na washabiki kufanya vurugu kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) iliyomalizika hivi karibuni.

Uamuzi
huo umefanywa na Kamati ya Mashindano ya TFF iliyokutana juzi (Juni 23
mwaka huu) jijini Dar es Salaam kupitia masuala mbalimbali ikiwemo
taarifa za mechi, na malalamiko kutoka kwa baadhi ya timu zilizoshiriki
RCL iliyochezwa katika vituo vya Mbeya, Morogoro na Shinyanga.
Town
Small Boys ya Ruvuma imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa kanuni
ya 37(13) ya Kanuni ya RCL kutokana na udanganyifu kwa kumtumia
mchezaji Agaton Mapunda ambaye hakustahili ingawa usajili wake
ulithibitishwa na TFF, kwa kutokuwepo pingamizi kutoka klabu yoyote
katika kipindi cha pingamizi.
Licha
ya usajili wake kuthibitishwa na TFF, Kamati ilibaini mchezaji huyo
hakutoka ndani ya Mkoa wa Ruvuma kama kanuni za RCL zinavyoelekeza. Hata
hivyo, matokeo ya mechi hiyo dhidi ya Njombe Mji iliyomalizika kwa bao
1-1 yanabaki kama yalivyo kwa mujibu wa kanuni ya Kanuni ya 52 (3 na 4)
na 31(11) ya RCL kwa kuwa mchezaji Mapunda alithibitishwa na TFF
(qualified player).
Vilevile
mchezaji huyo amepigwa faini ya sh. 200,000 kwa mujibu wa kanuni za
48(4) na 31(11) za RCL. Nayo malalamiko ya Njombe Mji dhidi ya mchezaji
David Noel Makakala kuwa ndiye aliyecheza mechi hiyo badala ya Carlos
Mapunda yametupwa kwa kukosa vielelezo na ushahidi wa kuthibitisha hilo.
Kiluvya
United FC ya Pwani imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa mujibu wa kanuni
ya 37(1) kutokana na vurugu za washabiki wake kwenye mechi namba 46
dhidi ya Abajalo iliyochezwa mjini Morogoro.
Pachoto
Shooting Stars ya Mtwara na Mshikamano FC ya Dar es Salaam zimepigwa
faini ya sh. 500,000 kila moja kwa kufanya vurugu kubwa kwenye mechi yao
namba 100 iliyovunjika mjini Morogoro. Pia Mshikamano FC wamepewa
pointi tatu na mabao matatu kwa mujibu wa kanuni ya 23(1na5) na 22(d).
Wachezaji na viongozi wa Pachoto Shooting na wachezaji wa Mshikamano FC waliofanya vurugu na kupigana, suala lao linapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa uamuzi na hatua za kinidhamu.
Wachezaji na viongozi wa Pachoto Shooting na wachezaji wa Mshikamano FC waliofanya vurugu na kupigana, suala lao linapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa uamuzi na hatua za kinidhamu.
Nayo
Tanzanite ya Manyara imefungiwa kucheza mashindano yote rasmi kwa msimu
mmoja, na kuteremishwa daraja hadi ligi ya wilaya mara itakapomaliza
kifungo chake kwa mujibu wa kanuni ya 21(3)(a), 37(14) na 22(a).
Tanzanite iliadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 23(1,5 na 6) baada ya
kumpiga mwamuzi kwenye mechi dhidi ya AFC na baadaye kugomea mchezo.
Ilishindwa kulipa faini na kujitoa mashindanoni kwa kuondoka kituoni.
Wachezaji wanaotuhumiwa kumpiga mwamuzi mpaka kumjeruhi suala lao litapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF.
Kamati
imetupa malalamiko ya African Sports ya Tanga dhidi ya Abajalo ya Dar
es Salaam, Ujenzi FC ya Rukwa dhidi ya AFC, Panone FC ya Kilimanjaro
dhidi ya Volcano FC ya Morogoro, na Mvuvumwa FC ya Kigoma dhidi ya Mbao
FC ya Mwanza kwa kukosa vielelezo na ushahidi.
Pia
malalamiko ya Mvuvumwa FC dhidi ya Geita Veterans ya Geita juu ya
kuwachezesha Ibrahim Alphonce, Zamoyoni Magoma na John Mtobesya kwa kuwa
hawakusajiliwa yametupwa kwa vile wachezaji hao ni halali, isipokuwa
orodha ya wachezaji wa Geita Veterans FC iliyotolewa kwa ajili ya
pingamizi ilikuwa na upungufu kiuchapaji ambapo wachezaji sita
hawakuorodheshwa
Nao makamishna Edward Hiza na Jimmy Lengwe waliokuwa kituo cha Morogoro wamepewa onyo kutokana na ripoti zao kuwa na upungufu.
vilevile Kamati ya Mashindano imezitangaza rasmi timu za African Sports, Geita Veterans na Panone FC kupanda kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015
vilevile Kamati ya Mashindano imezitangaza rasmi timu za African Sports, Geita Veterans na Panone FC kupanda kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015
Post a Comment