Kwa mujibu wa BBC,
Mwanamke wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa kosa la kuikana imani ya dini
yake na kuolewa na mwanaume anayempenda wa kikristu amechiwa kutoka
gerezani.
Shirika la habari la Suna limeripoti kuwa, hukumu ya kifo
iliyotolewa kwa mwanamke huyo Meriam Ibrahim ilibadilishwa na mahakama
ya rufaa.
Mwanamke huyo aliolewa na mwanaume wa kikristu na alihukumiwa
kifo kwa kutumia sheria za kiislamu baada ya kukataa kurejea kwenye
dini yake.
Mume wake amesema kuwa anatarajia kumuona mke wake akirejea nyumbani.
Aliwekwa gerezani tangu February mwaka huu akiwa na mtoto wake mdogo wa kiume aliyejifungua akiwa ndani.
Post a Comment