MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI “PRESS CONFERENCE” TAREHE 19.06.2014.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATU
WAWILI WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA
YA SAA 04:30 ALFAJIRIWALIONEKANA NA WALINZI WA USIKU WA ENEO LA SOKO KUU
LA TUNDUMA LILILOPO KATIKA KATA NA TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA
WAKIWA NA SILAHA BUNDUKI NA KUWATILIA MASHAKA KUWA WANA NIA YA KUFANYA
UHALIFU YAANI UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA.
WALINZI
AMBAO WALIKUWEPO KATIKA ENEO HILO WALITOA TAARIFA KWA ASKARI POLISI
WALIOKUWA DORIA AMBAO WALIFIKA MARA MOJA KATIKA ENEO HILO. KUTOKANA NA
TAARIFA HIZO MSAKO MKALI ULIANZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA HAO.
MNAMO
MAJIRA YA SAA 05:00 ALFAJIRI YA LEO ASKARI POLISI WALIKUTANA NA WATU
WAWILI WALIOWATILIA SHAKA KUTOKANA NA JINSI WALIVYOVAA KULINGANA NA
MAELEKEZO YALIYOPEWA NA WALINZI. MMOJA KATI YA MAJAMBAZI HAYO ALIKUWA
AMEVAA JAKETI KUBWA JEUSI NA MWINGINE AKIWA AMEBEBA MFUKO MKUBWA, WAKATI
WAKIJARIBU KUWASIMAMISHA WATU HAO WALIANZA KUKIMBIA NA MMOJA KATI YAO
ALIYEKUWA AMEVAA JAKETI ALIPOFIKA UMBALI WAMITA 20 ALITOA SILAHA BUNDUKI
NA KUANZA KUFYATUA RISASI OVYO AKIELEKEA UELEKEO WA ASKARI.
BAADA
YA KUONA HIVYO, ASKARI WALIJIBU NA KATIKA MAJIBIZANO HAYO
YA KURUSHIANA RISASI KATI YA MAJAMBAZI NA ASKARI POLISI, JAMBAZI MWENYE
SILAHA ALIPIGWA RISASI UBAVUNI NA KUFARIKI DUNIA, HIVYO KUFANIKIWA
KUKAMATA BUNDUKI MOJA AINA YA AK- 47 YENYE NAMBA 592058 IKIWA
NA RISASI 25 KWENYE MAGAZINE.
MTUHUMIWA
MMOJA ALIFANIKIWA KUKIMBIA NA MARA BAADA YA KUUPEKUA MWILI WA MAREHEMU
KILIKUTWA KITAMBULISHO CHA MPIGA KURA CHENYE JINA JOSEPH THADEI KAPINGA,
MKAZI WA MAFIGA, MOROGORO ALIYEZALIWA MKOA WA RUVUMA – SONGEA
VIJIJINI TAREHE 07.09.1971.
KATIKA
TUKIO HILO, HAKUNA MADHARA KWA WANANCHI/ASKARI YALIYORIPOTIWA KUTOKEA,
UPELELEZI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUMTAFUTA MTUHUMIWA ALIYEKIMBIA
PAMOJA NA MTANDAO WAO WA UJAMBAZI.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAMKE
MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA SUZANE MHENDWA (45) MKAZI WA UHAMILA
WILAYANI MBARALI AMEUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI NA MTU ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA LAZARO KATENDE.
TUKIO
HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 01:00 KATIKA
KITONGOJI CHA CCM, KIJIJI CHA UHAMILA, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA
YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI MZOZO
ULIOTOKEA KATI YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA WAKIWA NYUMBANI AMBAPO KIINI
CHAKE KINACHUNGUZWA.
MAREHEMU NA MTUHUMIWA NI NDUGU WANAOISHI NYUMBA MOJA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISIAHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII/WANAFAMILIA KUTUMIA NJIA ZA BUSARA KATIKA
KUTATUA MIGOGORO KATIKA FAMILIA HASA KWA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO
ILI KUEPUKA MATATIZO. AIDHA ANATOA WITO KWA MTU YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA
MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA TATU:
WATEMBEA
KWA MIGUU WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. THERESIA
HINGI (65) NA 2. MARY KIZITO (26) WOTE WAKAZI WA IGURUSI WAMEFARIKI
DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA BASI LA KAMPUNI YA USAFIRISHAJI – NEW FORCE
LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 952 CGU AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA
NA YAHAYA ABDALAH (39)MKAZI WA DSM.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 18.06.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONIKATIKA
KIJIJI CHA IGURUSI, KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO, BARABARA KUU YA
MBEYA/NJOMBE, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA BASI HILO
LILILOKUWA LIKITOKEA DSM KUELEKEA MBEYA MJINI LILIGONGA GARI T. 954 AMH
AINA YA FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA TUPA ANYOSISYE (32) MKAZI
WA KIWIRA –TUKUYU, KISHA KUACHA NJIA NA KUWAGONGA WATEMBEA.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO WATU WENGINE WANNE WALIJERUHIWA KATI YAO ABIRIA
MWANAUME MMOJA NA WANAWAKE WATATU WATEMBEA KWA MIGUU WOTE WAMELAZWA
KATIKA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA. PIA MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA
HOSPITALINI HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA DEREVA WA BASI,
AMBAYE AMEKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISIAHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
HASA KWA KUZINGATIA ALAMA NA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA
MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
Post a Comment