Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imeikataa rufani ya Michael Wambura kupinga kuenguliwa kugombea urais
katika uchaguzi wa klabu ya Simba unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi
huu.
Wambura
aliwasilisha rufani yake mbele ya Kamati hiyo iliyokutana leo (Juni 19
mwaka huu) jijini Dar es Salaam chini ya Kaimu Mwenyekiti Wakili Mwita
Waissaka kupinga uamuzi wa kumwengua katika kinyang’anyiro hicho
uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba kwa kufanya kampeni kabla ya
muda uliopangwa.
Baada
ya kupitia vielelezo, kanuni na sheria, Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya
TFF imeridhika kuwa mrufani (Michael Wambura) alifanya kampeni kabla ya
muda kinyume na Ibara ya 6(1)(a) na (g), Ibara ya 6(1)(l) pamoja na
Ibara ya 14(3) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.
Kwa
mujibu wa ibara hizo, Kamati ya Uchaguzi ya Simba inayo mamlaka ya
kumwengua (disqualify) mgombea anayefanya kampeni ama kukiuka maagizo
halali ya Kamati ya Uchaguzi.
Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF imeziagiza kamati zote za uchaguzi za
wanachama wa TFF kufuata kanuni za uchaguzi kama zilivyoainishwa katika
Katiba zao ili kuepusha rufani za mara kwa mara.
Uamuzi wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF umezingatia Katiba ya TFF pamoja na kanuni zake, na pia Katiba ya Simba.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Post a Comment