Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UKATILI MWINGINE .... BABA AMCHOMA MOTO MIKONO YOTE MIWILI MTOTO WA MIAKA 8 KWA KOSA LA KUCHELEWA KURUDI NYUMBANI

 





Mtoto mmoja wa  miaka nane, mkazi wa Mjimwema Songea mkoani Ruvuma amefanyiwa ukatili wa kutisha na Baba yake wa kambo aitwaye Stan Nyoni kwa kumchoma moto mikono yake yote miwili kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani.

Jeshi la polisi mkoani Ruvuma bado linamsaka mtuhumiwa wa unyama huo,Stan Nyoni ambaye alitoroka baada ya kufanya unyama huo huku mtoto huyo akiwa amelazawa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma Songea.



Tukio hilo la kinyama  limewafanya baadhi ya madaktari na manesi wa hospitali hiyo kumwaga machozi kutokana na mtoto Nice kufanyiwa kitendo hicho cha kusikitisha cha kuchomwa moto mikono yake miwili na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake.

Afisa muuguzi msaidizi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma Bw. Aidan Ndunguru anasema mtoto huyo  ameumia katika jicho la kulia,mgongoni huku  akiwa na majeraha makubwa katika viganja vya mikono yake miwili ambayo alimwagiwa mafuta ya taa na kuchomwa moto.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top