Ndugu Wanahabari.
Tafadhali
pokeeni Taarifa yetu kwa umma ya wajumbe wa mkutano mkuu wa CHADEMA,
BARAZA KUU, WAJUMBE WA BAVICHA NA BAWACHA kutoka mikoa mbali mbali hapa
nchini. tuliyoisoma mchana wa leo tarehe 23.6.2014 LAMADA HOTEL DSM.0756767672
TAARIFA
YA WAJUMBE WA BARAZA KUU NA MKUTANO MKUU WA CHADEMA KWA UMMA.
A. UTANGULIZI
Ndugu wanahabari.
Mbele yenu ni viongozi
halali wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kutoka mikoa yote ya Tanzania kwa uchache tumekutana jumla
ya wajumbe 78 kuwakilisha wenzetu
walioshindwa kufika kwa sababu mbali
Sisi ni wajumbe wa Baraza
Kuu na mkutano mkuu wa Chama ambapo pamoja nasi tumejumuika na wenyeviti wa
mabaraza ya WANAWAKE WA MIKOA YA TABORA
NA SINGIDA, MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA TABORA pamoja na MUASISI WA CHADEMA
kutokea mkoa wa SINGIDA na mwenyekiti wa M4C wilaya ya SINGIDA hivyo tunafanya jumla ya tuliokutana kwa
jambo hili kuwa ni wanachadema 82.
Tumewaita kuwaeleza namna ambavyo tumekuwa
tukisononeshwa na mwenendo wa chama chetu kwa kipindi kirefu sasa, hivyo
tunaomba mtusaidie kuufikishia umma mawazo ya wanachadema tunaowawakilisha huko
mikoani tutokapo.
B. KUSHINDWA KWA UONGOZI WA KITAIFA.
Tunasikitika kuona kwamba
kadri siku zinavyoenda Uongozi wa juu wa chama unazidi kushindwa kufanya kazi
ya kukiimarisha chama.
Baada ya jitihada
tulizozifanya kwenye uchaguzi wa 2010 sehemu mbali mbali, ni dhahiri ushindani
kwa sasa ungekuwa mkubwa sana kiasi cha chama kushika dola uchaguzi ujao iwapo
chama kingejikita kwenye jitihada za ujenzi wa chama.
Badala yake uongozi wetu
umewasaliti Watanzania waliokuwa na tumaini kubwa sana na chadema na kuwekeza
nguvu nyingi sana kwenye Kuimarisha migogoro baina ya viongozi wakuu wenyewe
kwa wenyewe, wanaimarisha ubinafsi miongoni mwa wanachama, wanaimarisha Udini
na Ukabila pamoja na ubadhilifu wa mali za chama.
Matendo haya ya viongozi
wetu ni UNAFIKI wa kisiasa, kiasi cha kutumia mabilioni ya shilingi kwenda
kumshambulia ama kummaliza kisiasa kiongozi mwenzao (Zitto Kabwe) na kuacha
ujenzi wa chama ukiendelea kuporomoka.
Kwenye ujinga huu, hakuna wa
kumlaumu zaidi ya Mwenyekiti wetu Freeman
Mbowe na na Katibu Mkuu Dkt.Wilbrod Slaa. Hawa wanafaa sasa
kuhukumiwa na watanzania wanaopenda mabadiliko ya kweli kwa kurudisha nyuma
jitihada za kuwakomboa na kukiimarisha chama na badala yake wamekuwa wakitumia
nguvu kubwa na rasilimali nyingi za chama kujiimarisha wao wenyewe.
Ndugu WanaHabari.
Mtakumbuka kwamba baada ya
uchaguzi wa mkuu wa mwaka 2010 ruzuku ya chama iliongezeka kutoka million 56
mpaka milioni 239 kwa mwezi.
Tunasikitika kuona kwamba
mpaka sasa chama kimeshindwa kufanya uwekezaji wenye tija ili kukisaidia chama
kiweze kujiendesha bila kutegemea Ruzuku ama kukopa kutoka kwa Mbowe kama
mwenyewe anavyopenda tuwe tunafanya.
Mpaka sasa chama kimepokea
jumla ya shilingi BILIONI 10.038
kama ruzuku kutoka serikalini ili chama kijiendeshe. Ni narudia, mpaka sasa
chama kimepokea kutoka serikalini jumla ya SHILINGI BILLION KUMI, NA MILIONI
THELASINI NA NANE.
Cha kusikitisha kwa kipindi
chote hicho na kiasi chote hicho cha pesa zitokanazo na kodi za waTatanzania pesa
ambazo zinasababishwa na kazi kubwa tuliyoifanya ya kukipigania chama kwenye
uchaguzi mkuu wa 2010, leo chama hakina hata jengo moja la OFISI MIKOANI KOTE
na OFISI zote za mikoa tunapanga kwenye FREMU za maduka na hata Pango la fremu
hizo tunajilipia wenyewe kwa kuchangishana, Mbowe na Slaa wanatumia MABILIONI
HAYA KURUKA NA CHOPA sisi huku chini tunaendelea kumenyeka kwa kigezo cha
UKAMANDA ,huu ni utumiaji mbaya wa mali za chama.
Tunasikitishwa sana na
kitendo cham mwenyekiti MBOWE kusema
anajilipa madeni aliyokikopesha chama kila siku, kiasi cha zaidi ya MILLIONI 700 Mbowe anajilipa kama madeni aliyokikopesha chama. Sasa
tunashindwa kuelewa deni hili ni deni gani lisiloisha?, na je deni hili
alikikopesha chama kwa mkataba gani?, na aliusaini mbele ya nani huo mkataba wa
mkopo?, Taratibu za chama kukopa zipo wazi je zilifuatwa?. Haya ni matumizi
mabaya ya fedha za umma.
Tunasikitishwa na kitendo
cha mwenyekiti mbowe kukiuzia chama MAGARI CHAKAVU kwa zaidi ya million 600,
Huku akijua ni chakavu na kwamba kabla ya kukiuzia chama alikuwa anakikodisha
magari hayo
Masikitiko yetu ni kitendo
cha MBOWE kununua LANDCRUISER V8 VX 2 kwa pesa za chama na kasha kuja kukiuzia chama,
lakini kama haitoshi mpaka leo hii Gari hizo zimesajiriwa kwa majina ya MBOWE
HOTELS. Haya ni matumizi mabovu mno ya mali za umma na kwamba yampasa sasa
ajitathmini kama anapaswa kuendelea kuwa kiongozi mtetezi wa wanyonge ama
mnyonyaji wa wanyonge.
Tunahudhunishwa na kitendo
cha Dkt. SLAA kutufanyia huduma ya kutuuzia ukombozi, haiwezekani kwa akili ya
kawaida, ukawa katibu mkuu unayelipwa zaidi ya million 130 kwa mwaka na chama
halafu makatibu na viongozi wako wa mikoani wanalipwa 0 kwa mwaka. Huu ni
udalali na unafiki wa kisiasa.
Mpaka sasa viongozi wakuu
hawa, wamevunja katiba ya chama kwa mambo makuu matatu yafuatayo.
1. Kitendo cha kutoka na kususia kwenye Bunge la
katiba bila kuruhusiwa na vikao halali vya chama.Bunge la katiba lilikuwa ni mazao ya Juhudi zetu sisi wanaCHADEMA tuliopambana nchi nzima kuidai katiba.
Chama chetu kilikuwa na fursa kubwa ya kutuwakilisha kwenye kuandika katiba hiyo na kufanya marekebisho makubwa kwa kadri tulivyoazimia.
Lakini kususa Bunge la katiba lililotokana na Sheria mliyoishiriki kuitunga, ni kutufanya sisi sote tunaowakilishwa na viongozi hawa tuonekane ni majuha.
Kwa kuwa CHADEMA ni miongoni mwa waasisi wa mchakato huu wa Katiba. Ni kuwasaliti Watanzania na kuikosesha nchi fursa ya kuandika katiba kususa.
2. Kitendo cha Kuunda Baraza Kivuli la mseto na vyama tulivyowaaminisha watanzania kuwa vina ushirika na CCM.
Kwenye hili, chama kinapaswa kuelezwa kama mazingira yaliyowafanya wenzetu hawa kuungana na CCM yamebadilika ama bado yapo?, Chama kinapaswa kuelezwa na mbowe na Slaa kuwa Uteuzi wa Mbatia kuwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais wa CCM umebatilishwa ama la?.
Lakini chama pia kitueleze kama Nafasi ya juu ya viongozi wa CUF kwenye serikali ya mseto na CCM kule Zanzibar haipo tena. Vinginevyo viongozi wetu wote walioshiriki hili wanatakiwa wawajibike haraka iwezekanavyo.
3. Kutokuitishwa kwa mkutano wa Baraza Kuu. Katiba yetu inatuagiza Kuwa Baraza kuu la chama litaitishwa kila baada ya miezi kumi na mbili. Kwa kuwa baraza kuu la mwisho liliitishwa February 2013, kulipaswa kuitishwa tena baraza kuu lingine kabla ya mwezi February 2014 kuisha.
E. AGIZO
·
Tunawaagiza viongozi wetu waitishe haraka
MKUTANO WA BARAZA KUU ili pamoja na mambo mengine viongozi wetu wajieleze mbele
ya Wajumbe ni kwanini Tusiwachukulie hatua za kinidhamu kwa makosa ya UBADHILIFU, KUSALITI NDOTO ZA WATANZANIA, na KUHAMASISHA MGAWANYIKO NA UBAGUZI NDANI YA CHAMA.
·
MBOWE na Dkt. SLAA wanatakiwa wajipime
wenyewe kama ni sahihi chama kukodi HELKOPTA (CHOPA) 3 na kutumia
zaidi ya BILIONI 1.4 za ruzuku
ambazo ni kodi za Watanzania halafu eti tunashinda KATA TATU kati ya zaidi ya KATA
27, Yaani kila HELKOPTA MOJA
imeleta KATA MOJA ama kila SHILINGI MILLIONI 466.6 kwa KATA MOJA, halafu chama hakionyeshi kushtuka
wala Kujali
·
MBOWE na Dkt. SLAA wajipime zaidi kama
wanafaa kuendelea kuwa viongozi wa chama huku chama kikizidi kudidimia kila
uchao kiasi cha KUDHARIRISHWA KWA kupata KURA 2000 CHALINZE na KURA 5000
KALENGA huku chama kikitumia zaidi ya MILLIONI 600 kushiriki CHAGUZI HIZO.
Imesomwa leo 23.6.2014 kwa niaba ya wajumbe nami;-
ATHUMANI
H. BALOZI
…………………………..
0756767672
KATIBU
WA CHADEMA MKOA WA TABORA
MJUMBE
BARAZA LA MASHAURIANO KANDA YA MAGHARIBI
MJUMBE
WA MKUTANO MKUU CHADEMA TAIFA.
Post a Comment