Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kibaya wilayani Kiteto ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa vyama vingi vya siasa vimekuwa kama wasanii wa kuigiza havina sera na vimekuwa vikiishi kutokana na matukio.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Kibaya wilayani Kiteto wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mpira wa Kibaya.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akichagua Tshirt ya Chama kutoka kwa wakina Mama Wajasiriamali wanaouza nguo za CCM wilayani Kiteto.
Nguo za CCM zimekuwa zinauzwa katika kila kona nchini na kuvaliwa na watu wengi ambapo inakadiriwa CCM ina wanachama zaidi ya milioni sita nchi nzima na idadi imekuwa ikiongezeka siku hadi siku.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanakijiji cha Irkiushbor wakati wa mapokezi mpakani mwa wilaya ya Simanjiro na Kiteto.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiruka juu kama Morani wa Kimasai alipotembelea kjiji cha Partimbo Eseki na kukagua miradi ya maji.
Wanakijiji cha Kimotoro wilayani Simanjiro wakizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kumuomba awasaidie kumaliza migogoro ya ardhi kati ya wafugaji na hifadhi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Partimbo Eseki baada ya kukagua miradi ya maji ambapo aliwataka wananchi hao kuitunza miradi hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi kutoka kwa wakina mama wa kijiji cha Partimbo kata ya Eseki .
Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kuwasaidia ng'ombe wa kijiji cha Partimbo kata ya Eseki wilayani Kiteto kunywa maji.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsaidia Mama wa Kimasai kumtwisha ndoo ya maji mara baada ya kuzindua huduma ya maji safi na salama, Kijiji cha Partimbo kata ya Eseki kina mradi wa maji kwa matumizi ya binadamu na mifugo.
Post a Comment