Jana usiku wadau wa filamu na vipindi vya TV walipatwa na mshituko baada ya kupata taarifa kuwa muongozaji mahiri wa filamu na vipindi vya runinga, George Tyson amefariki katika ajali ya gari.
DJ Choka alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa kwenye msafara mmoja na
timu ya The Mboni Show na marehemu George walioelekea Dodoma kutoka Dar
es Salaam Alhamisi (May 29) na kurudi wote (May 30).
Akiongea na tovuti ya Times Fm na kipindi cha Bongo Dot Home, DJ
Choka ameelezea safari yao ya kwenda Dodoma ambapo kipindi hicho
kilienda kutoa msaada wa madawati katika shule moja ya msingi.
Hii ni sehemu ya maelezo ya DJ Choka:
“The Mboni show ilikuwa inaenda kugawa madawati katika shule ya
primary iko Chamwino inaitwa Cheula kama sijakosea.
"Majira ya saa nane tukaanza safari ya kurudi Dar. Kwa hiyo mimi nikawa kwenye gari ambalo nilipanda mimi, Mboni na mama Mboni ambaye mimi namuita bibi na dereva.
"Majira ya saa nane tukaanza safari ya kurudi Dar. Kwa hiyo mimi nikawa kwenye gari ambalo nilipanda mimi, Mboni na mama Mboni ambaye mimi namuita bibi na dereva.
“Lakini gari lingine alilokuwa amepanda marehemu lilikuwa na watu
nane, cameraman wetu pamoja na sound engeneer, dereva na wengine ni
fans wa The Mboni Show. Tuliwapita sisi…tuliwaovertake maeneo ya Gailo,
tukawa tumeshafika Gailo mjini lakini wao walikuwa wanakuja. Kama kuna
mtu anaetoka Dodoma analijua hilo eneo la Gairo kuna kamlima fulani
halafu kama kana bonde.
“Kwa hiyo tairi lilianza kupiga pancha…tairi la upande wa kulia
la nyuma. Baada ya kupiga pancha tairi la nyuma dereva akayumba akawa
anaenda kama upande wa kulia, lakini upande wa kulia ikawa inakuja
pikipiki ikabidi aikwepe pikipiki asiigonge akawa anataka aende upande
wa kushoto.
"Sasa kwenda upande wa kushoto ndio pale tairi mbili za upande wa kushoto zote zikapiga pancha. Sasa ile mawengewenge na nini jamaa akafunga break, kufunga break gari ndio ikaingia pembeni ikageuka mara nne, mara ya tatu sijui marehemu ndio akawa ametoka kwenye roof kwa sababu yeye alikuwa hajafunga mkanda!

Kuhusu watu waliokuwa kwenye gari hilo na hali zao:
“Wengine ambao walikuwa wamekaa kwenye siti moja na marehemu ndio
ambaye amekuja kufuatwa na ndugu zake amewahishwa muhimbili.
"Kulikuwa kuna rafiki wa Mboni dada mmoja hivi nimemsahamu jina yeye alikuwa amekaa katikati ya marehemu na yule ambaye amepelekwa Muhimbili anaitwa Niko…huyo mvulana.
"Huyo dada yeye amevunjika mkono. Halafu hao wa nyuma sasa kama ukiitazama hiyo gari kwenye website yangu, nyuma kule…wale wameumia lakini sio sana.

“Kuna mama anaitwa Kipompapompa, sisi tunamuita Akisi, alikuwa
amekaa mbele…yeye alikuwa amefunga mkanda na dereva. Yeye hakupata
jeraha kubwa au nini zaidi ya kuwa analalamika kichwa kinamuuma.”
DJ Choka ameeleza pia kuhusu mwendo wa magari hayo mawili yaliyokuwa
yakiongoza na inaonesha kuwa gari alilokuwa amependa marehemu lilikuwa
nyuma ya gari alilokuwa amepanda DJ Choka na Mboni wakati ajali hiyo
inatokea.
“Tulikuwa tunaendesha gari kitaratibu tu yaani ile wao wanatupita
tunawapa nafasi, yaani tunaendesha gari kitaratibu tu zile za…yaani
mimi nakuovertake na wewe unaniovertake. Sisi tukawa tumesema muda huu
saa tisa/saa kumi tusije tukachelewa kuingia basi tukasema tutembee na
100 au 120.
"Lakini sisi tulipowapita tukapata simu, simu ikapiga bana sisi tumepata ajali. Ndio tukageuza hapo hapo wakati tuko katika maeneo ya Gailo hapo mbele.”
"Lakini sisi tulipowapita tukapata simu, simu ikapiga bana sisi tumepata ajali. Ndio tukageuza hapo hapo wakati tuko katika maeneo ya Gailo hapo mbele.”
Msikilize hapa akieleza kiundani:
credit : times fm
Post a Comment