Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAJANGA HAYA ... MCHUNGAJI ADAIWA KUMTOROSHA BINTI WA WATU HUKO KINONDONI...!

MCHUNGAJI mmoja wa kanisa la kiroho la Biblical lililopo Kinondoni jijini Dar es Salaam (jina tunalo), anadaiwa kumtorosha mwanamke aitwaye Catherine Paul (28) ambaye ni mfanyabiashara wa duka Tegeta jijini Dar.
Picha ya Catherine Paul anayedaiwa kutoroshwa na mchungaji.
 Habari zinadai kuwa, wakati akiendelea na biashara hiyo, Catherine alipata ugonjwa wa ajabu ambapo alionekana mnyonge. “Tunasikia alimshirikisha rafiki yake wa karibu, Victor ambaye alimpeleka katika kanisa la mchungaji huyo kwa ajili ya kuombewa,” alisema baba mdogo wa  Catherine,  Paulo Makaranga.
Iliendelea kudai kuwa baada ya kuombewa, Catherine alibadilika na kuanza kuonesha tabia za ajabu kama vile kutopokea simu hata alipopigiwa na mama yake mzazi.
Pia alikuwa akiacha duka lake wazi kwa madai kuwa anawahi kanisani, kushika Biblia kila mara, kukaa bila kula, kuwa mkimya na kikubwa zaidi ni kitendo cha kushinda kanisani siku nzima bila kufanya shughuli yoyote nyingine.
 Naye dada wa Catherine, Grace alipozungumza na gazeti hili juzi alisema aliwahi kwenda kanisani hapo kumuulizia ndugu yake akaambiwa anaishi kwa muumini mmoja.
Alisema alipofika kwa muumini huyo, alimkuta mkewe ambaye alisema amemchoka Catherine na kumtaka dada huyo achukue vitu vyake na aondoke navyo.
“Mke wa yule muumini alidai na yeye alinitafuta kwa kipindi kirefu kwa vile alimchoka mdogo wangu kwa mambo yake ya ajabu. Nilipomuuliza yupo wapi ili niondoke naye akasema amerudi kanisani,” alisema Grace.
Grace alisema alipofika nyumbani aliichambua mizigo ya Catherine na kukuta daftari lililoandikwa na Catherine mwenyewe maandishi  yakisomeka: 

‘Wazazi wako walishakufa, mimi nimekuwa baba yako wa kimwili na kiroho hivyo hakuna mtu wa kukuhukumu zaidi yangu na hakuna kuondoka kwenda bila ruhusa yangu na hata ukifa nitakuzika kwenye kanisa langu. Kuanzia leo wewe ni Irene na si Catherine.’
“Nilishtuka sana, nikaamua kurudi kanisani kwa mchungaji. Nilipofika waumini wake walinizuia kuingia kwa sababu walishajua mimi ni dada wa Catherine. Nikawaambia nahitaji kuombewa wakaniruhusu. Nilipoingia ndani sikuamini, nilimuona Catherine akiwa amekonda sana huku nywele zake zikiwa hovyo tena akionekana hana afya. 
“Kilichonishangaza nilimuona amesimama madhabahuni akiwa na mchungaji. Baada ya maombezi nilimfuata na  kujitambulisha ambapo alikasirika sana na kukataa kunisikiliza,” alisema Grace.
Grace aliongeza kuwa aliamua kumtaarifu mama yake Catherine,  Agatha Thomas na baba yake mdogo, Paulo Makaranga ambapo wote walitokea mkoani Tabora.
 

Baada ya kufika walitoa taarifa Kituo cha Polisi Kawe ambapo mchungaji huyo alidaiwa kufika hapo na kukiri kuwa kweli alikuwa na Catherine na kudai kwamba kwa muda huo alikuwa Mbeya hivyo angemrudisha. 
Aprili mwaka huu, binti huyo alirudishwa nyumbani kwako, Tegeta lakini ilipofika Juni 18, mwaka huu alitoroka tena na inasadikiwa amerudi kwa mtumishi huyo wa Mungu kwani walikuwa wakiendelea kuwasiliana.
 Alipotafutwa mchungaji huyo kuzungumzia sakata hilo, alidai yeye ameshamruhusu Catherine achague kama ataendelea kubaki kanisani hapo au awafuate wazazi wake na kusema kuwa Catherine mwenyewe aliamua kubaki.
“Catherine ni mtu mzima, yeye mwenyewe ameamua kuchagua kubaki kanisani badala ya kwenda na wazazi wake, sasa mimi kama mchungaji nifanye nini haya ni masuala ya kifamilia tu,” alisema mchungaji huyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top