Kutia
alama mwilini umekuwa utamaduni kwa miongo kadhaa katika maeneo tofauti
barani Afrika ili kuashiria urithi wa kikabila.Vitendo hivi hata hivyo
vinapungua lakini bado kuna watu wanaotaka kuendeleza kilichofanya na
mababu zao.Katika mji wa Ouidah kaskazini mwa Benin, kuna tambiko
inayotarajiwa kufanyika ikifuatwa na siku mbili za sherehe.Houeda ni
mojawapo wa makabila nchini Benin inayoamini kuwa tendo la kuchanja
watoto – hasa usoni- huwaunganisha na mababu zao.
Watoto
hao hupewa majina mapya, wananyolewa vichwa vyao na kupelekwa katika
makazi ya watawa ambapo kuna mizimu inayowasaidia kuzungumza na vizazi
vya hapo awali.
'Utamaduni unaoenziwa'
“Hii
ni sehemu ya tamaduni zetu na ni muhimu sana kwangu,” anasema Genevieve
boko, ambaye mwanawe wa kike mwenye umri wa miezi 6, Marina, pamoja na
wapwa zake Luc na Hospice wenye umri wa miaka 10 na miaka 12 wote wako
tayari kuchanjwa.
Post a Comment