Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi akionyesha silaha aina ya Ak 47 kwa Waandishi wa Habari Ofisini kwake |
Jeshi la
Polisi Mkoani Mbeya limeua Mtuhumiwa wa ujambazi Joseph Kapinga Mkazi wa Mafiga Mkoani
Morogoro akiwa na silaha aina ya Ak 47 yenye risasi 25 kwenye magazine.
Tukio hilo
limetokea June 19 mwaka huu majira ya saa 11 alfajiri ambapo askari
polisi walikutana na watu waliowatilia shaka kutokana na jinsi walivaa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jiji hapa Kamanda wa Polisi Mkoani Mumbeya Ahmed Msangi
alisema kuwa taarifa za kuwepo kwa watuhumiwa hao wa ujambazi hao waliarifiwa na
walinzi wa soko kuu la Tunduma.
Amesema
mara baada ya kupata taarifa hizo askari waliokuwa doria walianza
msako mkali wa kuwatafuta watu hao.
Amesema
kutokana msako huo walifanikiwa kuwaona watu hao wawili wakiwa wamevalia
makoti makubwa meusi huku mwingine akiwa amebeba mfuko mkubwa
ambao ulikuwa silaha.
Kamanda
Msangi amesema mara baada ya kuwaona watu hao walisimamisha
ambapo walianza kukimbia na mmoja kati yao aliyekuwa amevaa jaketi
jeusi alikimbia kwa umbali wa mita ishirini na kuanza
kufyatua risasi hovyo huku akielekea eneo waliopo askari.
Amesema
mara baada ya kuona hali hiyo askari walijibu mapigo na katika
majibizano hayo ya kurushiana risasi mtuhumiwa Kapinga ambaye alikuwa
akitumia bunduki aina AK.47 yenye namba 592058 na yenye risasi 25
kwenye alikufa papo hapo.
Hata hivyo
Msangi amebainisha kuwa katika tukio hilo hakuna madhara kwa
wananchi wala askari yaliyotokea huku uchunguzi zaidi ukiendelea
kufanyika ikiwa ni pamoja na kuendelea kumtafuta mshukiwa mwingine.
chanzo;fahari news
Post a Comment