Kuna sheria mpya inatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge la Senet ambayo sheria hiyo itawaruhusu watoto kuanzia miaka 10 kupewa mipira ya kondomu na dawa za kupanga uzazi.
Sheria ya afya ya uzazi ya mwaka 2014 ambayo tayari ipo mbele ya Senet, inasema
kuwa elimu kwa watoto kuhusu afya ya uzazi na ngono wapewe watoto
pengine hata bila ya wazazi kutoa idhini.
Sheria hiyo imewasilishwa na Seneta mteule Bi.Judith Sijeny anayesema
kwenye pendekezo la mswada huo kuwa watoto wanaovunja ungo wapewe nafasi
yakutosha kupata habari kamilifu kuhusu elimu ya ngono na huduma za
kisiri ikiwa ni pamoja na habari za kutosha na orodha ya dawa za kupanga
uzazi na habari kuhusu ujauzito na uzazi wa mpango.
Muswada huo unaashiria
kwamba wanaovunja ungo ni walio kati ya umri wa miaka 10 na 17 ambao ni
wanafunzi kati ya darasa la tano na kidato cha tatu.
Post a Comment