Mapokezi sifuri: Wachezaji wa Ureno wakiwasili uwanja wa ndege wa Lisbon, lakini mapokezi hayakuwepo.
WACHEZAJI
wa Ureno wamewasali nyumbani kwao baada ya kutolewa kombe la dunia,
lakini hakuna aliyejishughulisha uwanja wa ndege kumpokea nyota wa nchi
hiyo Cristiano dos Santos Aveiro Ronaldo
Ureno
angalau walijitahidi kuliko England, kwasababu waliambulia pointi nne
katika nafasi ya tatu kwenye kundi lililokuwa na nchi za Ujerumani ,
Marekani na Ghana, lakini kutupwa nje haipunguzi machungu kwao.
Ronaldo
alishindwa kuonesha makali yake kama mchezaji bora wa sayari hii na
aliishia kufunga goli moja tu katika mashindano ya mwaka huu.
Lakini ukweli ni kwamba nyota huyo alisumbuliwa sana na majeruhi na haikuwa rahisi kwake kufanya maajabu
Anahitaji lifti? Cristiano Ronaldo aliachwa na kwenda zake kwao
Taxi kwa ajili ya Ronaldo! Portugal alipanda Taxi baada ya kususwa na mashabiki mjini Lisbon
Japokuwa kulikuwa na mashabiki kidogo wakiwasubiri wachezaji wao, lakini hali haikuwa kama kawaida. Kulikuwa na ukimya mwingi.
Post a Comment