Shambulizi la bomu la kujitoa mhanga, limetokea kaskazini mwa Nigeria
katika eneo la Yobe ndani ya ukumbi ambao mashabiki walikuwa wamejaza
kutazama mechi za kombe la dunia.
Hali ya tahadhari ilitangazwa katika majimbo matatu ikiwa ni pamoja
na Yobe huku washukiwa wa mashambulizi hayo wakiwa ni kundi la
wanamgambo wa Boko Haram.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema mshambuliaji wa kujitoa mhanga
alikuwa ndani ya gari ndogo iliyokuwa imetegwa bomu wakati watu
wakiangalia mechi kati ya Brazil dhidi ya Mexico Jumanne jioni.
Ukumbi ambao mashambulizi yamefanyika ni maarufu sana na mara nyingi watu wengi hupenda kwenda kuangalia matukio makubwa.
Hata hivyo, mamlaka nchini Nigeria ilitoa onyo kwa wakazi katika
baadhi ya maeneo kuepuka kukaa sehemu za mkusanyiko kipindi hiki cha
kombe la Dunia wakiogopa mashambulizi ya wapiganaji.
Wachambuzi wanasema kuwa vikundi vya wapiganaji wa Kiislam, ikiwa ni
pamoja na Boko Haram, wameelezea mpira wa miguu kama kitu kisichofaa
katika dini ya Kiislamu.
Post a Comment