Jeshi
la Polisi kitengo cha usalama barabarani Wilayani Kahama mkoani
Shinyanga limefanikiwa kuzua mgomo wa madereva wa mabasi yaendayo
mikoani ambao wanapinga kutozwa faini isiyohalali na Kufanyiwa
uzalilishaji na baadhi ya Askari wa kitengo hicho. Mabasi
yanayosafirisha Abiria Kutoka kahama kwenda mikoani leo yamegoma
kusafirisha abiria wakishinikiza serikiali kuingilia kati suala la faini
wanazotozwa na asikari wa jeshi la polisi kitengo cha usalama
Barabarani.
farajimfinanga.com imefika eneo lakituo kikuu cha
babasi mjini Kahama majira ya saa 12.30 asubuhi na kukuta mgomo huo
ukiendela huku madereva wakiwa hawapo katika mabasi yao hali
iliyosababisha kuwepo kwa msongamano.
|
Kaimu
mkuu wa kitengo cha usalama Barabarani Wilayani kahama Thomas Myonga
akiwa na maafisa wengine wa kikosi cha usalama barabarani pamoja na
waandishi wa Habari |
Kwa
mujibu wa Madelewa ambao hawakutaka kutaja majina yao wamedai, wamekuwa
wakipigwa faini na asikari wa mkoa wa Singida na huwalazimisha kulipa
faini kubwa ya zaidi ya Shilingi 200,000 huku stakabadhi ikiandikwa
shilingi 30,000 inayotambulika serikalini.
Wamesemaa pia wamekuwa
wakilazimishwa kupigwa picha mbele ya mabasi yao wanapokamatwa hata
kama wanaendesha mwendo mdogo na kwamba hubambikiziwa kesi, na kwamba
baadhi ya madereva wamefikishwa mahakamani kwa kubambikiziwa makosa pale
wanapogoma kutoa faini.
Aidha wanapinga kitendo cha ukatili
alichofanyiwa dereva Mwenzao wa basi la Princess Munaa Lenye No. T 183
CRW ambaye alivunjwa mkono na asikari wa kitengo hicho huko Mbezi Jini
Dar es Salaam baada ya kugoma kunyang’anywa leseni yake.
Hata
hivyo mgomo huo ulioanza saa kumi na mbili Asubuhi umedumu kwa
takribani saa mbili na baadaye kuanza kwa safari, huku ikielezwa kwamba
mgomo huo ulikuwa ni siri ya Madereva kwani Mawakala wanaokata tiketi
hawakuwa na taarifa.
Akizungumza wakati wa mgomo huo Kaimu mkuu
wa kitengo cha usalama Barabarani Wilayani kahama Thomas Myonga
aliwataka madereva kuendelea na safari zao kwani mgomo huo ni batili na
wanaweza kuzisababishia kapuni zao hasara kubwa endapo ambiria
watafungua Mashitaka mahakamani.
Amewataka madereva kufuata
sheria za kudai haki zao ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sehemu
zinazohusika ili masula yao yashughulikiwe pasipo kuleta athari yoyote.
Mgomo
huo wa madreva wa mabasi umefanyika katika Miji ya Kahama, Bukoba,
Mwanza, Msoma na Dar es Salaam huku taarifa zikisema licha ya mgomo huo
kumalizika ila kwa sasa maderewa wanaendesha kwa mwendo wa chini kupita
kiasi na kwa msongamano, hali inayozidi kuwachelewesha abiria.
|
Askari polisi wakiangalia hali ya usalama wa abiria kufuatia mgomo huo |
|
Abiria wakiendelea kutawanyika huku mgomo ukiendelea |
|
Abiria wakiwa bado katika hali ya Taharuki |
|
Mgomo ukiendelea |
|
Afande Toma akizungumza na abiria pamoja na Madereva mara baada ya suluhu ya mgomo kupatikana |
|
Mabasi yakianza kuelekezwa kutoka stand na kuanza safari |
|
Mabasi yakiendelea kuondoka kuelekea mikoani |
|
Mabasi yakiendelea kuondoka kuelekea mikoani |
|
Mabasi yakiendelea kuondoka kuelekea mikoani |
|
Post a Comment