Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema
haitambui kuondolewa kwa kipengele cha ukomo wa uongozi uliofanywa na Chadema
bila kufuata idhini ya mkutano mkuu wa chama hicho.
Mwaka 2006, Katiba ya Chadema ilifanya marekebisho
yaliyoruhusu wanachama kugombea uongozi bila ukomo wakati awali, waliruhusiwa
kugombea kwa vipindi viwili vya miaka mitano.
Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chadema, inasema kipengele hicho katika Ibara ya
6.3.2 (C) kiliondolewa kwenye katiba bila idhini na mkutano mkuu wa chama
hicho. Mutungi alisema baada
ya kupitia muhtasari wa kikao cha mkutano mkuu wa
mwaka 2006 suala la kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi halikuonyesha
kujadiliwa katika mkutano huo.Hata hivyo, akizungumza kwa simu jana, Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema kipengele hicho kiliondolewa kwa
vikao vya chama ambavyo ni wilaya na mkoa.
“Mjadala kuhusu ukomo wa uongozi ulishamalizika na
haujadiliwi tena, ulishapitishwa na vikao halali vya chama, mkutano mkuu
ulipitisha yale yaliyoamuliwa na vikao vya chini,” alisema Dk Slaa.
Hata hivyo, Jaji Mutungi alisema: “Chadema wamefanya
mabadiliko bila kufuata katiba”
Alishauri waitishe mkutano rasmi na halali kwa mujibu wa
katiba ya chama hicho ili waweze kurekebisha kasoro zilizopo.Alisema kama chama
hicho hakitarekebisha kasoro hiyo, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haiwezi
kuitambua ibara hiyo.Alisema ingawa hoja hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba ambaye sasa si mwanachama
wake, bado hoja hiyo ni muhimu na inahitaji kufanyiwa kazi.
“Ni vizuri mkaifanyia kazi hoja hiyo bila kujali kwamba
aliyeiwasilisha si mwanachama tena wa Chadema,” alisema katika barua hiyo
LISSU AFUNGUKIA SAKATA HILI ...
Dr.Wilbroad Slaa akigombea Uenyekiti wa Chadema naye Mhe.Mbowe akagombea Ukatibu Mkuu wa Chadema Uchaguzi ujao kuna tatizo?.
Hakika
chaguzi hizi zinazofuata, zitawarudisha Wasakatonge na Intarahamwe
wengi vijijini kwao kutoka Dar Es Salaam, hatutakuwa na cha swalia mtume
kwamba alikopa Benki za Umma wa Watanzania mamillioni ya Shillingi,
mali zake zote zitapigwa mnada, zikawasaidie Wanafunzi wanaoketi juu ya
mawe na akina mama wajawazito wanaojifungulia sakafuni kwa kukosa vitanda mahospitalinl huko majimboni.
Ikumbukwe
kwamba Chadema ni Chama Kikuu cha upinzani Nchini, hatua ya kuitwa
Chama Kikuu Cha upinzani Nchini ni 'Long Process' inayopitia matukio
mengi ambayo sio kirahisi tu kuishushia hadhi Chadema kwa matumizi ya
'Poor technics' kama hizi tunazoshudia sasa. Sisi hatuna wasiwasi hata
kidogo kwa sababu hawa ni watu wadogo sana.
Endeleeni
kuzitangaza Ilani, Falsafa, Sera na Itikadi za Chama chetu kama kawaida
popote pale mlipo, hizi ni dalili za wazi za anguko la watawala
wanaoamini kabisa kwamba uongozi wa kidemokrasia ni mtaji wa maisha ya
mhusika
Post a Comment