Loading...
Home » Unlabelled » MTANGAZAJI KIWANGO WA KITUO CHA RADIO TIMES FM CHA JIJINI DAR, KHADIJA SHAIBU ‘DIDA’ AFUNGA MTAA KWA FUMANIZI
MTANGAZAJI KIWANGO WA KITUO CHA RADIO TIMES FM CHA JIJINI DAR, KHADIJA SHAIBU ‘DIDA’ AFUNGA MTAA KWA FUMANIZI
Kutoka kwa gossip cop wetu makini na wakuaminika alieomba hifadhi ya jina lake ametueleza kuwa ndoa ya Dida haipo tena baada ya Dida kumfumania mumewe na dogo dogo. Chanzo hicho kimedai kuwa Dida alimfumania mume wake ambae ni mtangazaji Ezden Jumanne na ndoa imevunjika rasmi na Ezden Jumanne amepokonywa vitu vyote vya thamani alivyokua amepewa na Dida,kama gari,simu ya thamani na vingine.
"We yaani ulitokea ugomvi mkubwa balaa yaani nusu afe mtu,mbona kitaa kilikua kazi ! kipindi kile ilifunga kwa kigodoro sasa safari ilifunga kwa fumanizi" Chanzo hicho kilisema. Hii ni ndoa ya 3 kwa mwana dada huyo ambae aliwahi kusema kua na hii ikivunjika basi hata kaa aolewe tena,waswahili wanasema usitukane mamba kabla hujavuka mto, tayari bidada kashavunja ndoa 3 na kumfanya awe katika rekodi ya aina yake hapa mjini kwa umri alionao na idadi ya ndoa alizopitia.
"Nina mwonea huruma yule Ezden maskini hana kitu ni wale wakaka wanaolelewa hapa mjini,yaani ye alikua anavishwa,analishwa na pesa ya kutumia inatoka kwa mamaa Dida,chezea Dida wewe" Kiliongeza Chanzo chetu.
Pole sana Dida,Je una maoni gani juu ya hili ? na juu ya vijana wanaowekwa ndani na wamama wa mjini ?
Post a Comment