Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

PICHA ZA KWANZA: MAJERUHI ALIYEKUWA PAMOJA NA TYSON KWENYE GARI


Mmoja wa majeruhi katika ajali, Gladys Chiduo 'Mc Zipomba' akiwa chini ya uangalizi wa nesi katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro akipatiwa matibabu mapema leo.
Mc Zipompa akiwa amepumzika baada ya kupatiwa matibabu.
(PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE, MOROGORO/GPL)

GARI ALILOPATA NALO AJALI DIRECTOR GEORGE TYSON

Muonekano wa Gari alilopata nalo ajali Director George Tyson.
Kwenye hii safari, George Tyson (kulia) aliambatana na mtangazaji Mboni Masimba wa The Mboni show.
DJ Choka (kushoto), akiwa na marehemu George Tyson (kulia) wakiwa Dodoma enzi za uhai wake.
Marehemu George Tyson enzi za uhai wake.
Dj Choka ambae alikua kwenye safari moja ya Dodoma na Marehemu George Tyson, ameandika kwamba Marehemu alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma.
Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni ikiwa ni saa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.
Kwenye gari walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha ila wengine wamepata majeraha mwilini akiwemo dereva wa gari hilo ambapo kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro baadae asubuhi safari ya kurudi Dar es Salaam itaanza.
PICHA/HABARI KWA HISANI YA DJ CHOKA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top