Hatimaye
Malawi imepata Rais mpya baada ya mivutano ya kisheria kwa wiki nzima.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amesema kutoka mjini Blantyre kuwa
Profesa Peter Mutharika ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 36.4
ya kura zote akifuatiwa na Dr Lazarus Chakwera mwenye asilimia 27.8 huku
Rais anayemaliza muda wake Dr Joyce Banda akishika nafasi ya tatu kwa
asilimia 20.2 na Atupele Muluzi amekuwa wa nne na asilimia 13.7
Mwenyekiti
wa tume ya uchaguzi Jaji Mackson Mbendera amesema uchaguzi huo
ulikumbwa na changamoto nyingi lakini mwishowe nchi ni lazima ipate
kiongozi wake na kuwaomba wananchi kuwa na utulivu .
Awali
Jaji Kenyata Nyirenda wa mahakama kuu mjini humo jana usiku alitoa
uamuzi kuwa hawezi kuvunja sheria kwa kuruhusu tume iongeze muda wa
kuhesabu upya kura kwenye maeneo yenye utata.
Post a Comment