Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TEAM WEMA, TEAM KAJALA KUVUNJWA.....YADAIWA NDO CHANZO CHA UGOMVI WA WEMA SEPETU NA KAJALA



Makundi  mawili  hasim  ya  wasanii  wa  filamu  Bongo, Wema  Sepetu  na  Kajala  Masanja  yajulikanayo  kama  'Wema  Team'  na  'Kajala  Team'  yanatarajiwa  kuvunjwa  kwani  ndio  yameonekana  kuchochea  bifu  la  wawili  hao  ambalo  limekuwa  likionekana  kuisha  na  kuibuka  tena....

Akizungumza  na  mwanahabari  wetu, Kajala  amesema  kuwa  tatizo  lao  limekuwa  likichochewa  na  makundi  hayo  hasa  wanapotangaza  kusamaheana  na  kuzika  tofauti  zao  makundi  hayo  huibuka  na  kuanza  kutukanana, kitu  ambacho  huzusha  tena  hasira  zao....
"Siyo  siri, tatizo  letu  linachangiwa  na  hizi  team  ambazo  zipo  kwa  ajili  ya  kuongeza  matatizo.Tunafikiria  kuyavunja  kwani  kwa  sasa  yameonekana  kutokuwa  na  faida  zaidi  ya  kuzidisha  hasira  ambazo  tumekuwa  tukizizika  kila  tunapotangaza  kusameheana," alisema  Kajala.

Msanii  huyo  alisema  hawaoni  haja  ya  kuwa  na  makundi  ambayo  hayawatakii  mema  kwani  katika  maisha  kukosana  kupo  lakini  pia  kusameheana  ndo  jambo  la  busara  kwani  hakuna  aliyemkamilifu  hapa  duniani.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top