Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi hapa nchini Jaji Mstaafu Damian Lubuva (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari jana, kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa
Singida, Liana Hassan na kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Joseph
Mchina.
Na Hillary Shoo, SINGIDA.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi imeanza mchakato wa
uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura,kwa kuwashirikisha kwa karibu
waandishi wa habari hapa nchini.
Lengo la kuwashirikisha waandishi wa habari ni
kutokana na uwezo na hekima katika kupeleka taarifa na kuhamasisha jamii na
wananchi kwa ujumla kupitia vyombo vya habari.
Hayo yamebainisha jana mjini hapa na Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva
wakati akifungua mkutano na waandishi wa habari wa Mkoa wa Singida.
Jaji Lubuva alisema lengo ni kuhakikisha kuwa wale
wote wenye sifa za kuwa wapiga kura wanajitokeza kwa wingi katika vituo vya
kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
Aidha alisema kuwa Tume inatarajia kufanaya uboreshaji
wa Daftari la Kudumu wa Wapiga kura kwa awamu ya kwanza hivi karibuni kwa
kutumia Teknolojia mpya ya Biometric Vote Regstration ( BVR).
Alisema mfumo huo mpya ni wa kuchukua au kupima
taarifa za mtu za kibaiolojia au tabia ya mwanadamu na kuhifadhi katika kanzi
data kwa ajili ya utambuzi.
“Mfumo huu hutumika katika kumtambua mtu na
kumtofautisha na mwingine, ingawa tabia hizo za binadamu ziko nyingi, lakini
kwa ajili ya kuandikisha wapiga kura alama za vidole kumi vya mikono, picha na
saini ndizo zitachukuliwa na kuhifadhiwa kwenye Kanzi Data (Database) ya wapiga
kura.” Alisisitiza Jaji Lubuva.
Hata hivyo alisema kwa kutumia mfumo huu wa (BVR),
wananchi wote wenye sifa za kuwa wapiga kura na wale walio na kadi za mpiga
kura watatakiwa kuandikishwa upya.
Jaji Lubuva alisema mafunzo kwa Watendaji yanatarajiwa
kufanyika muda kuanzia Mwezi Julai mwaka hauu kabla ya zoezi la uboreshaji wa
Daftari kufanyiaka.
Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba uhakiki wa vituo
vya kuandikisha wapiga kura umeshafanyika na kwa sasa uandikishaji utafanyika
katika vituo vilivyo katika ngazi ya vitongoji, Vijiji na Mitaa. Kutokana na
utaratibu huu wa sasa vituo vya kujiandikisha vimeongezeka kutoka 24,919 hadi
kufikia vituo 40,015 ambavyo vimewekwa katika ngazi za Vitongoji, Vijiji na
Mitaa’. Alisema na kuongeza
“Ili kuwezesha kuwa karibu zaidi na wanancahi na
hivyo kupunguza malalamiko ya auambali wa vituo vya kujiandikisha na kuaongeza
mwamko wa kujiandikishwa na kupiga kura.” Alifafanua Jaji Lubuva.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida,
Joseph Mchina, alisema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya zoezi hilo katika
Manispaa yake yamekamilika na hivyo kuwa na vituo 154 badala ya 84 vya awali.
Post a Comment