Brazil itachuana na Chile huku Uholanzi ikimaliza udhia dhidi ya Mexico"
Kocha
wa Uholanzi Louis van Gaal amelishutumu shirikisho la soka duniani FIFA
kwa "kufanya hila" kwa jinsi linavyopanga ratiba ya michuano ya Kombe la
Dunia.
Wenyeji
Brazil walicheza mechi mbili kabla ya Uholanzi kucheza, lakini
watacheza tena baada yake katika mechi ya mwisho ya makundi, jambo
ambalo Van Gaal anadai sio la haki.
"FIFA inafanya hila hizi.
Sio jambo zuri," alisema Van Gaal ambaye huenda timu yake ikachuana na Brazil katika mechi za muondoano.
"Sio mchezo wa haki.''
''Nadhani katika Kombe la Dunia taifa linaloandaa mechi hizi hutendekezwa ."
watakaomaliza
katika nafasi ya kwanza katika kundi A walioko Brazil watachuana na
watakaomaliza katika nafasi ya pili katika kundi B siku ya Jumamosi,
huku atakayemaliza katika nafasi ya pili katika kundi A akimenyana na
atakayemaliza katika nafasi ya B siku itakayofuata.
Brazil waliilaza Cameroon 4-1.
Uholanzi
na Chile tayari wamekwishafuzu lakini Uholanzi iliongoza kundi hilo,
jambo ambalo limemfurahisha van Gaal ambaye amekiri kutaka kuepuka
kucheza dhidi ya Brazil katika mechi ya kwanza ya raundi ya muondoano.
"iwapo ningechagua mimi, nisingependa kucheza dhidi ya Brazil, ingawa Croatia na Mexico sio wapinzani dhaifu pia,".
Hata
hivyo, kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari alisisitiza: "ni sharti
tucheze ili kufuzu, sio kubaini na kuchagua wapinzani wetu. Ni FIFA ndio
iliyochagua saa za kuanza michuano.
"kuna watu kadhaa waliotoa maoni kuwa tutachagua wapinzani wetu. ."
Mkufunzi
huyo anayechukua hatamu Manchester United pia aliwashutumu marefa
katika mashindano hayo, ambao alisema walizawadi penalti "zisizo za
haki" dhidi ya timu yake katika mechi mbili za ufunguzi ambazo Uholanzi
waliibuka washindi dhidi ya Uhispania na Australia.
Katika matukio yote mawili, timu pinzani zilifunga na kuwalazimu Uholanzi kutoka nyuma na kushinda.
"tumeona
katika Kombe hili la Dunia kwamba penalti walizopewa wapinzani wetu
katika matukio mawili hazikuwa halali, hilo ni sawa - angalau kwa maoni
yangu," alisema.
"katiaka
matukio mawili tunapata penalti. Hakuna taifa ambalo limewahi
kushuhudia jambo kama hilo, kwa hivyo labda refa huyo [Bakary Gassama
kutoka Gambia] atafanya kazi nzuri.
Ninatumai tu kwamba FIFA imefuata utaratibu mzuri wa kuchagua."Chanzo BBC Swahili
Post a Comment