Waasi
wa madhehebu ya waislamu wa Kisunni nchini Iraq wameripotiwa kuchukua
uthibiti kamili wa kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta nchini
humo katika eneo la Baiji kaskazini mwa Baghdad.
Kiwanda hicho kilikuwa kimezingirwa kwa kipindi cha siku kumi huku vikosi vya serikali vikizuia shambulizi la waasi mara kadhaa.
Msemaji
wawaasi hao amesema kuwa kiwanda hicho sasa kitapewa usimamizi wa
makabila yanayoishi katika eneo hilo na kwamba mapambano ya kuuteka mji
mkuu wa Baghdad yataendelea.
Utekaji
nyara wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Baiji ni muhimu sana kwa
waasi hao iwapo watasimamia maeneo ambayo wameyateka kufikia sasa, hasa
kwa kutoa umeme kwa mji wa Mosul.
Wakati
huo huo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry, ameahidi
msaada mkubwa kwa jeshi la Iraq wakati wapiganaji wa Kisunni wakiendelea
na mashambulizi yao nchini humo. Alisema Waziri Mkuu, Nouri al-Maliki
na viongozi wengine wameahidi kuunda Serikali ya Umoja inayowashirikisha
wote ifikapo mwisho wa mwezi.
Daktari
Zuhair Al-Naher, msemaji wa Serikali ya Iraq ambaye pia ni mwanachama
wa chama tawala cha Waziri Mkuu Nouri al-Maliki, Islamic Dawa Party,
anasema kuwa anaamini kuwa Bwana Maliki ataunda Serikali ya
kuwashirikisha wote.
Bwana Kerry alikuja Baghdad kwa mambo mawili.
Kwanza
kabisa kumshinikiza Waziri Mkuu Nouri al-Maliki na viongozi wengine wa
kisiasa kuwa wanapaswa kuwa na Serikali mpya, pana inayofuatia uchaguzi
mkuu uliofanywa Aprili. Mamlaka yanapaswa kugawiwa Wasunni na Wakurdi
walio wachache na sio kwa Washia ambao ni wengi pekee.
Pili
Bwana Kerry alitaka kuhakikishia Serikali ya Iraq kuwa Marekani
itasaidia wanajeshi wa taifa hilo wanapendelea kupambana na wapiganaji
wa Kiislamu wa kundi la ISIS, ambapo wengi wao ni.Chanzo BBC Swahili
Post a Comment