Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WASTARA NAYE AONYESHA UBABE KWA DEREVA DALADALA

UBABE! Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Wastara Juma aliwahi kuzichapa kavukavu na dereva wa daladala baada ya kuoneshewa ishara ya matusi.
Ishu ilikuwa hivi, miaka miwili iliyopita jijini Dar, Wastara alikuwa na wasanii wenzake kituoni sasa daladala likapita karibu yao na kummwagia maji na alipojaribu kumwambia kistaarabu kwamba hakufanya ‘fea’, dereva huyo akamuoneshea ishara ya matusi.
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Wastara Juma.

Wastara uvumilivu ukamshinda, akamvaa dereva huyo wa daladala na kumkwida ndipo vurugu kubwa ilipotokea maana dereva huyo naye hakutaka kukubali, alianza kujibu mashambulizi kabla wasanii waliokuwa na Wastara hawajamuamulia.
Alipotafutwa Wastara na kuulizwa juu ya kisa hicho, alicheka sana na kudai alikumbushwa mbali:
“Hahahahahaha! Daah siku hiyo ilikuwa si mchezo alinimwagia maji tena yenye matope halafu namwambia ananitukana palikuwa hapatoshi kama tusingeamuliwa, angeipata.”

chanzo: gpl
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top