VIJANA
wawili Dominick Kombe (36) na Hebert Macheka (30) wamepandishwa
kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
kwa kesi ya kukamatwa na vipande 28 vya pembe za ndovu vyenye thamani ya
shilingi milioni 275.
Watuhumiwa
hao walikamatwa Juni 5 mwaka huu eneo la Tabata, Kisukulu jijini Dar
wakiwa na nyara hizo za serikali ambazo hazikuwa na kibali chochote
kinyume na sheria.
Kesi hiyo
inayosikilizwa na Hakimu Waliyarwanda Lema chini ya mwendesha mashitaka
wa serikali Ofmedy Msenga, imeahirishwa mpaka Julai 9 mwaka huu
itakaposikilizwa tena baada ya watuhumiwa kutotimiza vigezo vya dhamana.
(Habari: Haruni Sanchawa / GPL)
Post a Comment