Waziri Mkuu wa
Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari
nje ya Hotel ya Serena ambapo alihudhuria Mkutano wa Tano unaohusu
masuala ya Uchumi,kulia kwake ni mkurugenzi wa benki ya Dunia nchini
Ndugu Philippe Dongier
Mkurugenzi wa
Benki ya Dunia nchini Tanzania Philippe Dongier akizungumza na waandishi
wa habari kwenye ukumbi wa kivukoni Serena Hotel jijini Dar es Salaam,
akiwa pamoja na Mwandishi wa Mada Ndugu Jacques Morisset ambapo
aliwaeleza waandishi hao Tanzania ina nafasi kubwa ya kupanua wigo wa
ajira kwa kutengeneza mazingira ya kufanyia kazi yenye ubora hasa
kwenye miji inayokuwa kwa kasi hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira
kwa Vijana na Wanawake.
Mkurugenzi wa
Benki ya Dunia nchini Tanzania
Philippe Dongier akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
kivukoni Serena Hotel jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na Mwandishi wa
Mada Ndugu Jacques Morisset ambapo alikiri pamoja na kukua kwa uchumi
lakini bado uchumi haujafungua au kutengeneza ajira kwa wananchi .
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
WAZIRI
Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda amesema kuwa wakati umefika
wajasiriamali nchini wanaoendesha shughuli zao katika sekta isiyo rasmi
kuboresha shughuli zao ili waweze kuzirasimisha kwa ajili kuboresha
maisha yao na Taifa kwa ujumla.
Mheshimiwa
Pinda amesema hayo jana (leo) jijini Dar es salaam wakati wa Uzinduzi
wa taarifa ya Hali ya Uchumi wa Tanzania-Toleo la Tano iliyoandaliwa na
Benki Kuu ya Dunia.
Taarifa
hiyo inalenga kutoa Sera na hatua za kuchukua kuwezesha kupanuka kwa
biashara katika miji na majiji nchini kwa ajili ya kuongeza ajira zaidi
kwa wananchi na hasa vijana.
Aidha,
Mheshimiwa Pinda alitoa wito kwa vijana nchini kujiajiri katika sekta
mbalimbali kama vile kilimo na kukiendesha katika mfumo ulio rasmi ili
kiweze kuwakomboa katika maisha yao na kuwasaidia kupata ajira.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi
na Uganda Bwana Philip Dongier ametoa wito kwa watunga Sera nchini
kuweka msisitizo katika kuendeleza ukuaji wa viwanda ili kutengeneza
idadi kubwa ya ajira mpya na zenye tija kwa wananchi.
Bwana
Dongier aliongeongeza kuwa changamoto nyingi zinazowakabili
wajasiriamali wadogo katika kusaka ajira ni fursa zinazotokana na
mchakato wa kupanuka kwa haraka kwa miji huku makisio ya hivi karibuni
yakionesha kwamba ifikapo mwaka 2030 watanzania wengi watakuwa wakiishi
mijini kuliko vijijini.
Taarifa
ya Hali ya Uchumi ambayo huchapishwa mara mbili kwa mwaka na Benki ya
Dunia inaeleza kwamba kuna uwezekano wa uchumi wa Tanzania kuendelea
kukua asilimia 7 kwa mwaka.
Post a Comment