Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akipongezana na Balozi
Chales Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii
Tanzania TTB mara baada ya kuzindua rasmi SITE ya Maonyesho ya Kimataifa
Utalii ya Tanzania yanayojulikana kama Swahili International Tourism
Expo (SITE) kwenye hoeli ya Serena Mwisho ni mwa wiki, Maonyesho
hayo yatakayohusisha kampuni binafsi, taasisi za kiserikali kama Bodi
ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na washirika wengine katika sekta hiyo
yanatarajiwa kufanyika tarehe 1 mpaka 4 Oktoba, mwaka huu katika ukumbi
wa Mlimani City Dar es Salaam, Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya
Utalii Bi. Devotha Mdachi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES
SALAAM) Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akizungumza katika zinduzi huo wakati alipokuwa akisoma hotuba yake.
Wageni wlikwa mbalimbali wakiangalia jinsi mabanda yatakayotumiwa na washiriki wa maonyesho yatakavyokuwa. Balozi Chales Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB akimkaribisha Waziri Razalo Nyalandu ili azungumze na kisha kuzindua maoyesho hayo. Seraphin Lusala Mkurugezni wa Masoko na Mauzo Serena Hotel kulia akiwa katika hafla hiyo. Balozi Chales Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB kulia akiwa pamoja na wageni wengine katika hafla hiyo. Wageniwaalikwa mbalimbali wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea wakati wa hafla hiyo. Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Bi. Devotha Mdachi na kulia ni Beatrice Mwiru Ofisa Masoko wa bodi hiyo. Msanii Wanne Star kushoto na kundi lake wakitoa burudani katika hafla hiyo. Burudani kutoka kundi la Wanne Star ikiendelea wakati wa hafla hiyo Meneja wa Masoko Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena Katikati, Emmanuel Okware Meneja wa mauzo kutoka Quatar Airways kulia na mdau Juma Mabakila wakiwa katika hafla hiyo. Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akizungumza na Bi. Lima D'Silva Mwakilishi wa mauzo Ethiopian Airlines. Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akisalimiana na wageni mbalimbali waliohudhuria katika haf hiyo. Baadhi ya wanahabari wakiwa katika hafla hiyo Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo katika hafla hiyo Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Bw. Goefrey Tengenea wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na maofiza wenzake wa TTB wakati wa hafla hiyo.

................................................................................................
(HOTUBA YA MH. WAZIRI RAZALO NYALANDU WAKATI WA UZINDUZI WA SITE)
Napenda
kuchukua nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati, kwa wageni wote
mliofika katika tukio hili muhimu ambapo nitatambulisha kwenu kuanzishwa
kwa onesho jipya la utalii la kimataifa litakalojulikana kwa jina la
Swahili International Tourism Expo (S!TE).
1.
Sekta ya Utalii ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi hasa kwa
kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi kama vile usafirishaji,
viwanda na biashara, kilimo, sanaa za mikono na kadhalika. Sekta ya
utalii ina uwezo wa kuongeza ajira kwa haraka zaidi na inatambulika
kwamba kila mtalii mmoja anapokuwa nchini huchangia takribani nafasi 12
za ajira za aina mbalimbali. Aidha, Utalii ni tasnia muhimu katika
kuongeza kipato na kupunguza umasikini, kukuza mahusiano ya kijamii na
vile vile katika kutunza na kuendeleza maeneo ya kihistoria na
maliasili. Hapa nchini, katika kipindi cha kati ya mwaka 2002 na 2013,
utalii wa kimataifa umekuwa kwa zaidi ya asilimia 50%, kutoka watalii
575,000 mwaka 2002 wambao waliliingizia taifa Dola za Marekani milioni
730 hadi kufikia watalii 1,135,884 mwaka 2013 ambao waliingizia taifa
Dola za marekani Bilioni 1.81.
2.
Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na vivutio vya maliasili na utamaduni vya
kipekee. Kutokana na kuwepo kwa vivutio hivi, taasisi ya Kimataifa ya
World Economic Forum katika taarifa yake ya ushindani kwenye tasnia ya
Utalii (Travel and Tourism) imeitaja Tanzania kuwa ni nchi ya pili (2)
duniani ikiongozwa na Brazili kwa kuwa na mazingira asilia yenye Urithi
asilia wa kimataifa, wingi wa wanyamapori na ardhi kubwa iliyo
hifadhiwa. Hakika, ni ukweli usiopingika kwamba katika vivutio saba vya
maajabu ya asili katika bara la Afrika, vitatu vinatoka Tanzania. Huu ni
ushuhuda kwamba juhudi zetu za kuhifadhi mazingira zinazaa matunda.
Hivi sasa Bonde la Ngorongoro; hifadhi ya Taifa ya Serengeti, na Mlima
Kilimanjaro ni vivutio ambavyo vimeorodheshwa katika Maajabu saba ya
asilia barani Africa.
3.
Hata hivyo, hatuwezi kutegemea tu uwingi na ubora wa vivutio hivi vya
utalii peke yake. Ni muhimu kuongeza juhudi zaidi kuliko wakati mwingine
wowote, ili kujenga uelewa wa utajiri huu kidunia. Kama taifa,
tunahitaji juhudi na mikakati zaidi ili kutangaza vivutio vyetu.
4.
Kwa kuzingatia umuhimu wa kuendelea kutangaza utalii wetu na kuifaya
Tanzania iweze kushindana kimataifa, mnamo mwezi Februari, 2013, Bodi ya
Utalii Tanzania (TTB), iliingia makubaliano na kampuni inayojulikana
kama Pure Grit Project and Exhibition Management LTD, hapo mwanzo
ilijukana kama Witch & Wizard Creative (Pty Ltd) ili kuanzisha
maonyesho ya utalii ya kimataifa nchini Tanzania yajulikanayo kama
Swahili International Tourism Expo -S!TE), ambayo yataanza rasmi Mwezi
Oktoba, 2014. Pure Grit Project and Exhibition Management LTD ni kampuni
inayoendesha maonesho ya utalii ya INDABA ambayo ni maonesho ya tatu
kwa ukubwa duniani. Onesho la S!TE litafanyika hapa Dar es salaam, mwezi
Oktoba kila mwaka katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na kujikita
zaidi katika kuvutia washiriki kutoka ndani nan je ya nchi.
5.
Mkoa wa Dar es Salaam umechaguliwa mahsusi kuwa eneo la kufanyika kwa
onesho la S!TE kutokana na sehemu ulipo Mkoa huo kijiografia, na uwepo
wa miundombinu bora na huduma nzuri zinazofaa kwa kuendesha au kuanzisha
maonyesho ya utalii ya kimataifa.
6. Hadi kufikia Juni 2014, hali ya maandalizi ya onesho hili ni kama ifuatavyo.
6.1
Mwenendo wa idadi ya washiriki hadi sasa: Zaidi ya asilimia 50% ya
nafasi za maonesho hayo tayari zimejazwa kwa kuchuliwa na makampuni
binafsi na Bodi za Utalii za nchi mbalimbali. Aidha, kuna idadi kubwa na
ya kuridhisha ya maombi ya washiriki inayoendelea kuandaliwa. Lengo ni
kwamba ifikapo katikati ya mwezi Agosti, 2014 tuwe tumetumefikia
asilimia 100.
6.2
Programu maalum ya kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo mawakala
wakubwa wa biashara ya Utalii: Katika kuhakikisha kuwa onesho hili
linakuwa ni fursa ya kuwaunganisha wafanyibiashara ya Utalii wa Tanzania
na masoko ya Utalii, S!TE itakuwa na programu maalum (Hosted buyer and
travel writer programme) ya kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo
mawakala wakubwa wa biashara ya Utalii na waandishi wa habari za utalii
(Tour Operators, Wholesalers, Packagers and Travel Agents and Travel
Writers) na kuwapangia ratiba maalum ya kuonana na washiriki wa maonesho
hayo ili kuwawezesha kuanzisha uhusiano wa kibiashara. Mawakala hao
wapatao ishirini na wandishi wa habari kumi watagharimiwa (hosted) na
S!TE.Hadi kufikia Juni 2014,mawakala 13 kutoka Marekani, Australia,
Ujerumani, Uholanzi, India, Mexico, Norway na China wamethibitisha
ushiriki wao.
6.3
Utangazaji wa Onesho la S!TE: Onesho la S!TE lina tovuti ijulikanayo
kama www.site.co.tz. Tovuti hii imeandaliwa ili kukidhi maudhui ya
onesho lenyewe ambapo inataarifa nyingi zinazoweza kumfanya yeyote
anayetembelea tovuti hiyo kupata taarifa zote muhimu kwa muda mfupi. Kwa
mfano tovuti inatoa taarifa za ukumbi wa onesho, mabanda ya maonesho
yatayojengwa na kumruhusu mteja kuchagua eneo kulingana na uwezo wake.
Aidha, tovuti hii ambayo pia imeunganishwa na ukurasa wake wa Facebook,
inapatikana kwa lugha mbalimbali
7.
Pamoja na kuitangaza Tanzania kama kituo muhimu cha utalii katika
ukanda wa Afrika ya Mashariki, S!TE ina lengo la kuunganisha wafanya
biashara wa Utalii wadogo na wa kati wa Tanzania (Small and Medium
Tourism Enterprises - SME’s), na masoko ya utalii ya kimataifa. Ni
ukweli kwamba SME’s za kitanzania zina uwezo mdogo wa kimtaji wa kuweza
kufikia masoko ya utalii ya kimataifa. Kupitia S!TE, hasa kupitia
programu maalum ya kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo mawakala
wakubwa wa biashara ya Utalii, itasaidia katika kutatua changamoto hii.
Naomba watanzania kuchangamkia fursa hii muhimu katika kukuza biashra ya Utalii nchini.
Post a Comment