Mtandao wa Facebook umelaumiwa kwa kuwafanyia wateja wake utafiti wa kisaikolojia bila ya kuwajulisha.
Nia
ya utafiti huo ilikuwa kujua kama wateja wake wamebadili tabia ya
kuweka picha na mawazo yao katika mtandao huo kutokana na kukasirishwa
na tabia za baadhi ya watumiaji wenzao.
Utafiti
huo uliohusisha takribani watumiaji 700,000 unaonyesha kuwa Facebook
inacheza na taarifa za watumiaji wake ili kupata hisia zao katika kile
wanachokiweka kwenye mtandao huo.
Hata
hivyo mtandao wa Facebook umekanusha madai hayo na kwamba hakuna
mtumiaji binafsi aliyelengwa na utafiti huo uliofanywa na mtandao huo
kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Cornell na California.
“Ngoja
tuuite utafiti kama Facebook wenyewe wanavyouita, lakini ni dalili za
wazi za kushindwa kuzingatia maadili na nguvu ya kulinda haki za
watumiaji wake” amesema Kate Crawford katika ukurasa wake wa Twitter.
Waziri wa kazi Jim Sheridan
mjumbe wa bodi ya mawasiliano ameagiza uchunguzi kufanyikadhidi ya
mtandao huo wa Facebook katika tuhuma hizi.
Hata hivyo Katherine Sledge
Moore, Profesa wa Saikolojia katika chuo cha Elmhurst , Illinois
amesema kwa jinsi ambavyo Facebook wamekuwa wakishughulika na taarifa za
wateja wake makubaliano yaliyopo katika utafiti huo hadhani kama yapo
nje ya hali ya kawaida.
Adam
Kramer kutoka Facebook mmoja kati ya walioandaa taarifa ya utafiti huo
anasema wanadhani kuwa ilikuwa mhimu kwao kutafiti mashaka yanayowakumba
watumiaji hasa katika mawazo yanayowekwa na marafiki zao na jinsi
yanavyowafanya wafikirie tofauti .
BBC
Post a Comment