Wakati
mgumu unaendelea kuwa kumba wachezaji wa kikosi cha timu ya Taifa ya
Ivory Coast baada ya nyota wa tegemezi wa timu hiyo Yaya na Kolo Toure
kufiwa na mdogo wao wa kiume wakati ndugu hao wawili wakiwa katika kazi
ya kutetea Taifa lao kunako fainali za kombe la Dunia nchini Brazil.
Msiba huo
mkubwa kwa Yaya Toure pamoja na kaka yake Kolo Toure umetokea jana
jijini Manchester ambapo mdogo wao Oyala Ibrahim Toure alifariki akiwa
hosptali The Christie akipewa matibabu baada ya kuugua saratani.
Ibrahim
Toure amefariki akiwa na umri wa miaka 28 jana wakati kaka zake wakiwa
uwanjani wakitetea taifa lao licha ya kuambulia kufungwa kwa bao 2-1.
Tofauti
na msiba huo ambao umechoma mioyo ya Yaya na Kolo Toure pia mchezaji wa
timu hiyo ya Ivory Coast Serey Die jana masaa 2 kabla ya mchezo dhidi
ya Colombia kuanza alipokea taarifa za msiba wa baba yake na kufanya
mchezaji huyo kucheza akiwa katika wakati mgumu ki-fikra.
Klabu ya Manchester City imetuma salamu za rambirambi katika familia ya Toure kufatia msiba huo.
Katika maisha ya Oyala Ibrahim Toure amewahi kuzichezea klabu za
i. 2002-2003: ASEC Mimosas
ii. 2003-2006: Metalurh Donetsk
iii. 2006-2007: OGC Nice
iv. 2009-2010: Al-Ittihad Aleppo
v. 2010-2013: Misr Lel Mikasa
vi. 2012: Telephonat Beni Sweif (loan)
vii. 2013-2014: Al-Safa’ SC
i. 2002-2003: ASEC Mimosas
ii. 2003-2006: Metalurh Donetsk
iii. 2006-2007: OGC Nice
iv. 2009-2010: Al-Ittihad Aleppo
v. 2010-2013: Misr Lel Mikasa
vi. 2012: Telephonat Beni Sweif (loan)
vii. 2013-2014: Al-Safa’ SC
Bwana ameto, bwana ametwaa jina lake lihimidiwe………AMINA
Post a Comment