Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Vitambulisho vya Taifa vyaanza kugawiwa.

               

NIDA-June20-2014 5c618
Na Hudugu Ng'amilo
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza kugawa Vitambulisho vya Taifa kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa jana na Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, ilieleza kuwa huduma hiyo ilianza kutolewa juzi ikianzia katika wilaya ya Temeke.
Kata ambazo NIDA imeanza kugawa Vitambulisho ni Mtoni, Azimio, Tandika, Buza na Yombo Vituka ambapo katika kata hizi zoezi la ugawaji litafanyika Juni 18 hadi 22, 2014.
Ilieleza kuwa majina ya waombaji wa vitambulisho yamebandikwa kwenye mbao za matangazo za ofisi za Serikali ya Mitaa husika na kwamba waombaji wanatakiwa kwenda na risiti walizopewa na NIDA baada ya kuchukuliwa alama za vidole, kupigwa picha na kuweka saini ya kielektroniki.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, huduma inatolewa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni na kuwa Mamlaka inatumia njia mbalimbali za mawasiliano kuwafikia walengwa katika zoezi hili.
CHANZO: NIPASHE

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top