WAZIRI
Mkuu, Mizengo Pinda, ametangaza uamuzi wa Serikali wa kuunda Tume ya
Elimu, itakayoshughulika na ajira na nidhamu ya walimu, kukabili
changamoto zinazowakabili walimu nchini.
Alitoa
tangazo hilo jana bungeni mjini Dodoma, katika kipindi cha Maswali ya
Papo kwa Hapo kwa Waziri Mkuu, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa
Igunga, Dk Dalaly Kafumu (CCM).(Martha Magessa)
“Sasa
Serikali imekubali kuanzisha chombo maalumu, kitakachoshughulikia
nidhamu na ajira za walimu, tunatarajia kinaweza kutusaidia,” alisema
Pinda na kufafanua kuwa uanzishwaji wa chombo hicho umeshakubaliwa na
Baraza la Mawaziri.
Dk Kafumu
katika swali lake, alisema tatizo la malipo ya walimu ni la siku nyingi
, akataka Pinda aseme lini suala la deni la walimu litaisha.
Kutokana
na kuendelea kwa tatizo hilo, Dk Kafumu alisema wiki iliyopita walimu
katika jimbo analotoka la Igunga, waliandamana mpaka ofisi ya Mkurugenzi
wa Elimu (DED) na kumfungia ofisini, ingawa pamoja na hatua hizo, bado
hawajalipwa madai yao.
Akifafanua,
changamoto zinazowakabili walimu nchini, ambazo tume hiyo inatarajiwa
kuja kutoa ufumbuzi wake, Pinda alisema tatizo kubwa linatokana na
walimu kuhamia shule ambazo hawakupangiwa awali.
Pinda
alisema changamoto zinazowakabili walimu zipo za aina mbili, moja madai
ya posho zao na stahiki zingine na pili, tatizo la kukosa malipo mara
wanapoanza kazi.
Alifafanua
kuwa kinachochelewesha kupata malipo yao, ni tabia ya walimu kuhamia
shule ambayo hawakupangiwa, na majina yao yanapoingizwa katika mfumo wa
kielektroniki, mfumo huo unakataa kwa kuwa jina linakuwa katika shule
ambayo hawakupangiwa.
Aliwataka
walimu kuacha kuhama shule kienyeji, badala yake wafuate utaratibu kwa
kuhama kihalali, ili mfumo huo wa kielektroniki, utambue uhamisho wao.
Kwa
mujibu wa Pinda, kwa sasa kuna mfumo mwingine unaotumika, lakini pia huo
mwalimu akihama kienyeji, itachukua muda kwa mfumo huo kumtambua.
Hatua ya
Serikali kukubali kuundwa kwa tume ya elimu, kunatokana na baadhi ya
wabunge, kuhimiza uundwaji wa Tume ya Kudumu ya Elimu, itakayochunguza
mfumo wa elimu nchini.
Wabunge
hao walipigia chapuo tume hiyo, wakati walipokuwa wakichangia hotuba ya
Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka wa
fedha 2014/2015 iliyowasilishwa na waziri wake, Dk Shukuru Kawambwa.
Mbunge wa
Kuteuliwa, James Mbatia (NCCR Mageuzi), alisema; “Tumwombe Rais aunde
Tume ya Kudumu ya Elimu kwa sababu kwa hali inavyokwenda ni mbaya sana
na napendekeza Tume hii ishughulike na kudhibiti mambo yote yanayofanya
kutetereka kwa ubora elimu nchini”.
Chanzo;Habarileo
Post a Comment