Stori: Joseph Shaluwa
AFYA ya
mtangazaji mwenye jina kubwa Bongo, Aboubakar Sadik ambaye anatumikia
Radio One Sterio ya jijini Dar es Salaam, si nzuri kiasi cha kulazimika
kufanyiwa upasuaji haraka.
Habari
kutoka chanzo chetu cha kuaminika, zinasema kuwa, Abou alizidiwa ghafla
Jumamosi ya Julai 26, mwaka huu akiwa kazini kwake na kukimbizwa katika
Hospitali ya Hindu Mandal, Posta jijini Dar es Salaam.
“Alikuwa mzima kabisa, alizidiwa ghafla na kukimbizwa Hindu Mandal ambapo alifanyiwa upasuaji,” kilisema chanzo chetu.
Risasi
Mchanganyiko lilipotaka kujua aina ya upasuaji aliofanyiwa Abou, chanzo
kikafunguka: “Ndugu yangu, suala la ugonjwa ni siri ya mgonjwa na
daktari wake, labda uwasiliane naye, maana ametoka hospitali leo asubuhi
(Jumatatu), ana nafuu nzuri.”
Baadaye
mchana chanzo hicho kilimtumia picha mbalimbali za Abou akiwa
hospitalini hapo, ikiwemo aliyokuwa chumba cha upasuaji wakati shughuli
ikiendelea.
Mwandishi
wetu alipomtafuta mtangazaji huyo kupitia simu yake ya mkononi,
hakupokea hivyo akalazimika kumtumia ujumbe uliosomeka: “Pole kaka,
nimepata taarifa unaumwa. Nini zaidi? Unaendeleaje sasa?”
Muda
mfupi kabla ya kuelekea mitamboni, Abou alijibu: “Shukrani kaka. Ni
kweli, nilifanyia surgery (upasuaji) Hindu Mandal, lakini
nimesharuhusiwa, nashukuru Mungu ilikwenda vizuri.”
Abou anawika na vipindi mbalimbali Radio One vikiwemo Nani Zaidi, Chombeza Time, Mtaa wa Mangoma na Flavor 120.Chanzo GPL
Post a Comment