(Picha na Fahari News)
MTOTO, Brayani Emanuel mwenye umri
wa miaka sita, amenusurika kuuawa baada ya mama yake mzazi Rose Mwanisisi Mkazi
wa kitongoji cha Chemchem kilichopo eneo la Mbalizi Mbeya vijijini, kujaribu
kumchoma moto kwa kutumia mifuko ya manila.
Tukio hilo limetokea Julai 16 mwaka
huu, ambapo imeelezwa kuwa mama huyo baada ya kurudi nyumbani kwake majira ya
jioni hakumkuta mtoto,hivyo aliaanza kumtafuta na alipompata alimfungia ndani
na kisha kumchoma moto kwa kutumia
mifuko ya manila.
Fahari News lilifanikiwa kuzungumza
na mtoto huyo ambaye kwa sasa analelewa na Babu yake Emanuel Omary(61), alisema
mama yake alipomkamata alimuingiza ndani kisha alichukua mifuko ya
rambo(manila) na kumuwekea kwenye miguu yake.
Aliendelea kufafanua kuwa, baada ya
mama huyo kuweka mifuko ya rambo kwenye miguu alienda kuchukua kibatari na
kuanza kuunguza mifuko hiyo kwenye miguu yake licha ya mtoto huyo kuomba
msamaha.
“Mama alinikuta ninacheza na
wezangu mbali kidogo na eneo la nyumbani, alinichukua na tulipofika nyumbani aliniambia kwamba
amechoka na mimi hivyo leo atanifundisha adabu, ndipo alichukua mifuko ya rambo
na kibatari na kuanza kuniunguza kwenye miguu yangu,”alisema mtoto huyo.
Amesema, wakati mama yake akiendelea
na zoezi hilo la kumuunguza miguu kwa kutumia uji wa moto uliotokana na kuungua
kwa mifuko hiyo ya manila yeye aliendelea kupiga kelele za kuomba msamaha mpaka
majirani walivyofika na kumuokoa.
Post a Comment