Ujerumani wameipiga Brazil kipigo cha mbwa mwizi.
Na Baraka Mpenja
KWA Muda mrefu wananchi wa Brazil waliandamana wakipinga nchi yao kuandaa fainali za kombe la dunia kwasababu kiasi kikubwa cha fedha kimetengwa.
Walikuwa wakihuzunishwa na matumizi makubwa ya fedha kwa ajili ya kuandaa miundo mbinu ya kombe la dunia, wakati maisha yao yakiwa katika hali mbaya.
Huduma mbovu za jamii, umasikini wao uliwahamasisha kuandamana na kuleta sintofahamu ya kisiasa.
Brazil walienda kwa kujivuta na mnamo juni 12 mwaka huu wakasahau shida zote na kushuhudia timu yao ya Taifa ikicheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Croatia.
Walipata ushindi wa mabao 3-1 na kufurahia matokeo hayo.
Faraja pekee kwa wananchi maskini wa Brazil ilikuwa ni kuona timu yao inafanya vizuri na kubeba kombe. Walikuwa wanafurika uwanjani, kwenye kumbi za kuoneshea mpira, lengo ni kutaka kuona timu yao inafanya nini.
Brazil ambayo unaweza kusema ni mbovu kuliko Brazil zote zilizopita, ilijikongoja hatua ya makundi na kuingia hatua ya 16.
Baada
ya hapo walipigiwa mbungi kubwa na Colombia, lakini walifanikiwa
kusonga mbele kwa mikwaju ya penati na kutinga nusu fainali.
Kwa bahati mbaya wakiwa na ubovu wao, waliingia mikononi mwa `watu katili`, Ujerumani.
Kabla
ya mechi, kocha Luiz Felipe Scorali alijigamba kuifunga Ujerumani na
katika mkutano wa jana na waandishi wa habari alithubutu kuuzungumzia
mchezo wa fainali, tena dhidi ya Argentina.
Kwa bahati mbaya hakufirikiria kama anaenda kukutana na Ujerumani yenye bunduki zote.

Saa
hazigandi, majira ya saa 5 usiku, ngoma ikaanza katika dimba la
Estaduuio Mineirao, huku Neymar na Thiago Silva wakikosekana.
Kama masihara vile, Ujerumani walianza kuchezea nyavu za Brazil mapema.
Watu wakajua kawaida, lakini mvua iliyokuja kwa Wabrazil ikuwa kubwa mno.
Beki mbovu ya Brazil ilipitisha mipira mingi. Dante, Luiz, Marcelo, Maicon, daaah! siku ilikuwa mbaya kwao.
Watu wote waliovaa nguo za njano walitamani mpira uishe.
Brazil usiku huu imefungwa mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani katika mchezo wa fainali ya kwanza ya kombe la dunia.
Hii
ni rekodi mbaya katika soka la Dunia. Brazil inakuwa nchi ya kwanza
kufungwa mabao mengi zaidi katika hatua ya nusu fainali ya kombe la
dunia tangu lianze mwaka 1930 nchini Uruguay.
Mabao ya Ujerumani yamefungwa na Muller, 11, Klose, 23, Kroos, 24, 26, Khedira, 29, Schurrle, 69, 79.
Bao pekee la Brazil limefungwa na Oscar katika dakika za lala salama.
Post a Comment