Moto Mkubwa ambao umetumika kwaajili ya kuteketeza dawa Za kulevya.(Picha na Fahari news) |
MAHAKAMA
Kuu ya Tanzania Nyanda za Juu Kusini, imetoa amri ya kuteketeza moto dawa za
kulevya aina ya Heroin zikiwa na uzito wa Kilogram 34.664 zenye thamani ya
shilingi Bilioni 1.8 baada ya upande wa mashitaka kufunga kusikiliza utetezi wa
shauri hilo.
Dawa
hizo, zilikamatwa mwaka 2010, katika eneo la Tunduma mpakani mwa Nchi ya
Tanzania na Zambia zilidaiwa kusafirishwa na raia wawili kutoka nchini Afrika
Kusini, Vuyo Jack (33) pamoja na mkewe Anastazia Elizabeth.
Akitoa
amri hiyo, Jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania (Mbeya) Noel Chocha, alisema mahakama baada ya
kumaliza kutumia vielelezo hivyo kwenye kesi hiyo ya usafirishaji wa dawa za
kulevya ikiwa ni kinyume cha sheria sura ya 16 kifungu kidogo (i)(b)(i) kilichofanyiwa
marekebisho mwaka 2002 inaamuru kuteketezwa moto dawa hizo ndani ya saa moja
mara baada ya kuhairisha kusikiliza shauri hilo.
Awali, mahakama
hiyo ilishindwa kuteketeza vielelezo hivyo kutokana na mshitakiwa Vuyo Jack
kuiomba mahakama kuvitumia vielelezo hivyo wakati wa utetezi wa kesi yake ambao
umemalizika juzi.
Mahakama hiyo,
mara baada ya kufunga kusikiliza utetezi wa mshitakiwa huyo wa kwanza ilitoa
nafasi kwa mshitakiwa wa pili Anastazia Elizabeth, endapo nayeye angependa
kutumia vielezo hivyo kwenye utetezi wake unaotarajia kuanza, Julai 28 mwaka
huu ambaye alikataa kwa kuimbia mahakama ya kwamba hatavitumia.
“Hivyo kutokana
na mshitakiwa wa pili kukataa kutumia vielelezo hivi kwenye utetezi wake ni
vema vikateketezwa kwa kuchomwa moto ndani ya saa moja mara baada ya kuhairisha
shauri hili,”alisema Jaji Chocha.
Aidha, dawa
hizo zikiwa chini ya ulinzi mkali wa askari polisi zilitolewa ndani ya mahakama
na kusafirishwa mpaka kwenye eneo la tukio ambako wahusika walikamilisha
taratibu za uchomaji wa dawa hizo za kulevya kisha kuziteketeza kwa kuzichoma
moto.
Dawa hizo aina
ya Heroin ziliteketezwa kwa moto wa nyuzi joto 700 hadi 900 huku wahusika wote
wakishuhudia kukamilika kwa zoezi hilo, vikiwemo vyombo vya dola, waandishi wa
habari, baadhi ya wanachi wa eneo hilo na washitakiwa wenyewe.
Ili, kufahamu
ya kwamba zoezi hilo limefanyika vizuri bila ya kuacha shaka miongoni mwa watu,
wahusika walipatiwa elimu kutoka kwa wataalamu kwa kueleza alama za rangi ya
moto itakayoonekama wakati wa zoezi hilo likifanyika.
.
Hata hivyo
zoezi la uchomaji lilianza kwa mtaalamu kutupia pakti moja moja ndani ya moto
huo ukiwa na nyuzi joto kati ya 700 na 900 mpka vifurushi vyote 37
vilipomalizika.
Post a Comment