Stori: Musa Mateja
HUKU modo
maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’, akisota
jela nchini China kwa skendo ya kukamatwa na madawa ya kulevya (unga),
mrembo mwingine ambaye aliwahi kujaribu kuchomoka kisanii kwenye muziki
wa Kizazi Kipya almaarufu kwa jina la Winnie Mandela, naye amenaswa na
polisi nchini humo.
Mrembo almaarufu kwa jina la 'Winnie Mandela' katika muziki wa kizazi kipya akiwa amenaswa na polisi China.
Tukio
hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupitishwa kwa msako
maalum wa kutokomeza biashara hiyo katika viunga vya Mji wa Hong Kong,
China.
JUX, PETIT MAN WAPATA WAKATI MGUMU
Kwa
mujibu wa chanzo chetu chenye maskani yake Hong Kong, Mbongo Fleva, Juma
Khaleed ‘Jux Vuitton’ na meneja wa msanii wa Bongo Fleva aitwaye
Mirrow, Petit Man nao walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunusurika
kuunganishwa kwenye oparesheni hiyo ya ukamataji wa waingizaji wa
madawa ya kulevya nchini China.
MADAI YA KUBEBA UNGA
Ilidaiwa
kwamba Winnie alijikuta mikononi mwa askari wa China akidaiwa kubeba
mzigo wa unga tumboni hivyo kukamatwa na kutembezwa mitaani kuelekea
kituo cha polisi.
APITA VIZUIZI, AKAMATWA
Ilisemekana
kwamba Winnie ambaye ni msichana wa mjini Dar, alifanikiwa kupita
vizuizi vyote lakini kwa hali ilivyo kwa sasa nchini humo ndipo
akajikuta akikamatwa na kutembezwa mtaani kama mhalifu wa kivita.
“Unaambiwa
ilikuwa kama vita kwani polisi wa China huwa wana silaha za kutisha
sana. Unajua Winnie alikamatwa kwenye mitaa ambayo kuna Wabongo wengi
hapa Hong Kong,” kilisema chanzo chetu kutoka Hong Kong.
Ilidaiwa
kwamba askari hao walipokea agizo maalum kutoka kwenye kitengo cha
kudhibititi madawa ya kulevya nchini humo kwani kwa sasa nchi hiyo
imechafuka kwa uingizwaji wa madawa ya kulevya, jambo ambalo limeifanya
serikali ya China ifanye oparesheni kubwa ya kuhakikisha wanatokomeza
wimbi hilo.
KWA WABONGO CHINA
Chanzo
chetu kilisema kwamba kwa sasa Wabongo wanaokwenda au wanaokaa China
wanaishi kama digidigi kwani wamefikia hatua ya kutoonesha pasipoti zao
na hata wengine wanadiriki kukataa uraia wao kwa kuwa Wabongo ndiyo
wanasakwa kwa wingi.
“Sasa
hivi jamaa wakisikia huyo ni Mtanzania wanamfuatilia sana kwani ndiyo
wenye sifa ya uingizaji wa dawa za kulevya nchini China,” kilisema
chanzo hicho na kuongeza:
KAMA HUAMINI MUULIZE JUX AU PETIT MAN
“Hicho ndicho kilichomtokea Winnie. Nakwambia Wabongo wanazidi kukamatwa na madawa ya kulevya. Yaani ni aibu, huwezi kuamini.
“Wabongo wengi sana wamekamatwa Hong Kong na wengine familia zao Bongo hazijui.
“Kama Watanzania hawaamini wawaulize Jux na Petit Man ambao walishuhudia mtiti mwanzo mwisho.”
BALOZI WA TANZANIA CHINA
Ili
kupata undani na idadi ya Watanzania wanaokamatwa kwa ishu za madawa ya
kulevya nchini China, gazeti hili lilimtafuta Balozi wa Tanzania China,
Luteni General Abraham Shimbo ambapo simu yake ya ofisini iliita bila
kupokelewa.
Wakati
Jack Patrick akisubiri kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine mwezi
ujao, ripoti zinaonesha kwamba wapo Watanzania wengi waliofungwa na
wengine kunyongwa kwa msala wa madawa ya kulevya.Chanzo GPL
Post a Comment