DEREVA mmoja wa basi la Princes Munaa linalofanya safari zalke toka Mwanza-Dar, Bw. Hamidu Juma anadai kupigwa na Polisi Juni 26 mwaka huu huko Mbezi, Kimara jijini Dar.
Akizungumza na mwandishi wetu, Hamidu alisema “Basi letu lina
madereva wawili, zamu yangu ilikuwa imeisha, tulipofika Kimara tulikuta
foleni, nikaamua kushuka ili kutazama sababu ni nini, niliporudi
nikakuta basi letu liko pembeni likiwa limezungukwa na askari, baadhi
wakiwa na nguo za kawaida, walitaka kung’oa karatasi za bima na
zinginezo nikakataa ndipo wakadai nawafundisha kazi, wakaanza kunipiga
mpaka mifupa ya mkononi imepishana’’.
Aidha dereva huyo anadai hajavunjika ila
mifupa imepishana na pia ana uvimbe kwa hiyo amepewa siku saba ndipo
arudi kufanyia uchunguzi wa kina.
Post a Comment