ALIYEKUWA
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage, ameshusha pumzi na anakwenda
kupumzika huku akidai kuiacha Simba na mambo matatu ya kihistoria.Wakati
akiwa amekamilisha uongozi wake kwa klabu ya soka ya Simba, Ismail Aden
Rage amefafanua mambo makubwa matatu aliyoiachia klabu hiyo kabla ya
kukabidhi mikoba.Rage amesema cha kwanza kikubwa ni akaunti ya klabu
yenye kitita cha Shilingi milioni 420 , pili ni Uwanja wa Bunju na tatu
makubaliano yake na Benki ya Posta kuhusiana na kadi za wanachama
ambazo kama uongozi mpya utakuwa makini, klabu itaingiza pesa nyingi
kupitia mtindo huo.Akikokotoa kiasi hicho cha Sh420 milioni, Rage
alisema kati ya hizo zimo Sh60 milioni za mauzo ya Shomari Kapombe
aliyesajiliwa na Azam FC, Sh160 milioni za kodi ya mapango ya jengo la
Simba lililopo Kariakoo jijini Dar es Salaam na Sh100 milioni za
wadhamini.
Akizungumza
na Mwanaspoti pia Rage alionyesha hisia zake juu ya kero alizokuwa
anakutana nazo alipokuwa madarakani, alisema: “Kuongoza klabu kubwa
kama Simba ni lazima ujitoe, hata hivyo vurugu kubwa za klabu ambazo
zinatokea huwa zinasababishwa na njaa tu. Hivyo kumaliza muda wangu
nashukuru maana nakwenda kupumzika.
Post a Comment