Kamishna
wa tume ya taifa ya uchaguzi jaji John Mkwawa akizungumza na waandishi
wa habari wa mkoa wa Njombe kuhusu kupeleka elimu kwa jamii ili
wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari ya kudumu la wapiga
kura kwa mfumo mpya.
======
Tume
ya taifa ya uchaguzi imewataka wananchi wanaotakiwa kujiandikisha
kupiga kura kwa mujibu wa sheria, kujitokeza kwa wingi kushiriki katika
zoezi hilo ili waweze kupiga kura ya maoni ya katiba mpya pamoja na
uchaguzi mkuu 2015.
Kauli
hiyo imetolewa leo Julai mosi na Kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi
Mh. Jaji John Mkwawa katika ufunguzi wa mkutano wa tume hiyo na
waandishi wa habari mikoani uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya
Njombe mkoani Njombe.
Jaji
Mkwawa amesema hata kama wananchi wamejiandikisha toka awali na
wanavitambulisho, vitambulisho hivyo havitatumika tena na badala yake
mwananchi mwenye umri wa miaka 18 au zaidi atatakiwa kujiandikisha upya
kupitia teknolojia mpya ijulikanayo kama "Biometric Voter
Registration"(BVR).
Wandishi wa habari wakimsikiliza.
Mkurugenzi wa idara ya habari ya tume hiyo Bibi Ruth MashamHatua
hiyo imefikiwa na tume ikiwa ni njia mojawapo itakayosaidia kuboresha
daftari la kudumu la wapiga kura ikiwemo kuwaondoa wale waliojiandikisha
mara mbili, waliopoteza sifa kwa mujibu wa sheria, waliofariki, pamoja
na wale watakao hama vituo kabla ya siku ya kupiga kura
Jaji
huyo amewataka wananchi kujitokeza kujiandikisha upya hivi karibuni kwa
kuwa kazi ya kuanza kuandikisha wapiga kura nchini itaanza kufanywa kwa
jinsi tume ilivyojipanga, na yeyote aliye na sifa anatakiwa kushiriki
kwani kwa sasa idadi ya vituo vya kujiandikisha vimeongezeka hadi
kufikia ngazi ya vitongoji na mitaa ili kuwarahisishia wananchi.
Mkurugenzi wa idara ya habari ya tume ya taifa ya uch Bibi Ruth Masham akiongea na waandishi wa habari leo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa idara ya habari ya tume hiyo Bibi Ruth Masham
amesema tume hiyo kwa sasa imejipanga vilivyo kufikisha ujumbe huo
kupitia waandishi wa habari kote nchini, huku akiwasisitiza wanahabari
hao kufikisha elimu kwa jamii ili lengo la wananchi wote wenye sifa
waweze kujiandikisha.
Amesema
matumizi ya mfumo huo mpya wa BVR utatumiwa kwa shughuli za uchaguzi tu
na si vinginevyo ambapo alama zote za vidole 10 vya mikono, saini
pamoja na picha ndivyo vitakavyochukuliwa wakati wa uandikishaji.
"Zoezi
hili linashirikisha wote wenye mika 18 na zaidi, wale wenye ulemavu
mfano hawana vidole vyote upo utaratibu mzuri ulioandaliwa, wote
watapatiwa vitambulisho.
Mwanahabari Lilian Mkusa wa gazeti la daraja letu mkoani Njombe akiuliza swali
Gabriel Kilamlya kutoka Uplands fm akiuliza swali lake.
Wakijiandaa kujibu maswali
Waandishi
hao wa habari mkoa wa Njombe walioshiriki katika mkutano huo wameahidi
kushirikiana na tume ya taifa ya uchaguzi kufikisha ujumbe huo kwa jamii
huku wakionesha kufurahishwa na tume kuwashirikisha mapema(kuwafanya
watu wa kwanza) kukutana nao kabla ya wadau wengine
Post a Comment