Chelsea wamethibitisha kumsajili rasmi Diego Costa baada ya kufikia makubaliano na Atletico Madrid.
Chelsea ilitaka kukamilisha usajili huo kabla ya
Kombe la Dunia kwa pauni milioni 32. Jambo
hilo halikufanikiwa lakini sasa mkataba umefikiwa. Taarifa iliyotolewa
imesema: "Chelsea inathibitisha kufikia makubaliano na Atletico Madrid
kwa ajili ya uhamisho wa Diego Costa".
Chelsea walikuwa wamekubali kulipa ada ya
uhamisho na Diego Costa mwenyewe aliwaambia Atletico hamu yake ya
kuondoka, lakini mkataba ulikuwa mgumu kufikiwa.
Post a Comment