Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

FAHAMU SABABU YA VAN GAAL KUBADILI KIPA


Kocha wa Uholanzi Luis van Gaal amesema urefu wa kipa Tim Krul ndio ulimfanya amchezeshe katika mikwaju ya penati katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Costa Rica.
Krul, mwenye urefu wa futi 6 na inchi 4, (mita 1 sentimita 93) aliingia badala ya kipa aliyeanza Jasper Cillessen zikiwa zimesalia sekunde chache kabla ya mikwaju ya penati kuanza kupigwa. Jasper ana urefu wa futi 6 inchi 2 (Mita1 sentimia 87).
Krul aliweza kupangua penati mbili, na hivyo Uholanzi kushinda kwa magoli 4-3.
 Tulidhani kuwa TIm ndio kipa bora wa kuzuia penati, Ni mrefu na ana nafasi zaidi ya kuzuia.
Menenja huyo wa Manchester United aliongeza kusema:
 Ilifanikiwa, ilienda vyema. Ninajivunia kidogo kwa hilo.
Uholanzi, timu pekee kati ya nne zilizosalia ambayo haijawahi kushinda Kombe la Dunia, itapambana na Argentina mjini Sao Paulo siku ya Jumatano. Brazil itacheza na Ujerumani katika nusu fainali ya kwanza siku ya Jumanne.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top